Kuzuia umwagaji Damu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuzuia umwagaji Damu

Question

Kwa namna gani makundi ya Kigaidi yalipuuza suala la kuzuia umwagaji damu.

Answer

Kwa kweli makundi ya kigaidi yalipuuza makusudio makuu yaliyokuja nayo jumbe na vitabu vya mbinguni, yakiwemo kuilinda nafsi na kuchunga utukufu wake, zaidi ya hayo, wafuasi wa makundi haya waliwahukumu watu ukafiri kwa tuhuma yoyote au shaka, jambo lililosababisha kumwaga damu za wengi wasio na hatia kama tunavyoona katika hali halisi ya siku hizi na siku zilizopita katika historia ya makundi haya ambapo wamezoea kuwaua, kuwatisha na wasio na hatia kikatili, wakihalalisha kumuua asiyewaunga mkono na kufuata fikra zao baada ya kumhukumu ukafiri, ingawa Sharia ya kiislamu ilisisitiza uharamu wa kupoteza nafsi na kumwaga damu, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: "aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote" [Al-Ma’idah: 32], Ibnu Abbas amesema: aliyemuua mtu mmoja akakiuka utukufu wake basi huwa sawa na aliyewaua watu wote, pia Mtume (S.A.W.) amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Amekuagizeni kuchunga damu, mali na heshima zenu isipokuwa kwa haki" (Imesimuliwa na: Al-Bukhary), vile vile, Mtume amesema: "kwa kweli kuangamizwa kwa dunia nzima kwa Mwenyezi Mungu ni rahisi zaidi kuliko kuawa muumini pasipo na haki" (Imesimuliwa na: Ibnu Majah), hivyo Sharia ya kiislamu iko tofauti kabisa na madai na jinai za magaidi hao.

Share this:

Related Fatwas