Kurudisha mfumo wa Khilafa wa kiisl...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kurudisha mfumo wa Khilafa wa kiislamu

Question

Ni nini maana ya khilafa? Ni ipi sura yake katika zama za kisasa? Je, inapaswa kusimamisha mfumo wa khilafa kama wanavyodai wenye msimamo mkali? 

Answer

Khilafa: ni kuwa na nafasi ya mtungaji wa sharia kwa lengo la kuhakikisha manufaa ya dini na dunia.

Khalifa: ni yule anayechukua nafasi ya aliyekuwa kabla yake, Wanachuoni wengi wanaona kuwa khilafa ni mfumo wa kiidara wa kutawala, kuendesha na kusimamia nchi ambao katiba za kisasa zimechukua nafasi yake, kwa hiyo hakuna haja ya kurudisha mfumo huu wa khilafa kwa maana yake ya zamani kwa kuwepo katiba, ambapo mfumo huo ulikuwa unafaa wakati ule, licha ya kwamba si nguzo mojawapo ya nguzo za dini ambazo Waislamu wanapaswa kuisimamisha kwa sura yake ya zamani, Wanachuomi wengine wanaona kuwa Waislamu wanatakiwa kufanya juhudi za kurudisha mfumo wa khilafa kwa umbo lake la zamani, kundi la tatu la Wanachuoni  wanaona kuwa mfumo huo wa khilafa unaweza kuhuishwa katika umbo la "muungano wa kijamhuri"; ambapo manufaa mengi yapatikane kwa nchi za Kiislamu pamoja na kila mtawala kuwa na madaraka yake kamili.

Lakini makundi ya kigaidi yanajiwajibisha na wafuasi wake kusimamisha na kurudisha khilafa na kuainisha khalifa miongoni mwao kwa namna ya zamani ya kuchagua khalifa, jambo ambalo likawafanya baadhi ya vijana kuasi serikali zao na kutoka kutaka kurudisha mfumo wa khilafa, wakaona kuwa Hadithi zilizokuja katika kukataza kumwasi mtawala haziwalenga wale wanaojitahidi kurudisha khilafa kwa hivyo wakatoka mbali na mafunzo ya sharia na mantiki sahihi.

Ukweli ni kwamba khilafa ilikuwa mfumo wa kiidara na wa kisiasa wa kupanga masuala ya dini na dunia katika nchi ya Kiislamu, na kwa kuwa mifumo ya kisasa inakidhi mahitaji hayo hayo basi hakuna sababu ya kupigana na kuuana kwa ajili ya mambo ambayo yapo lakini kwa namna tofauti na yale wanayoyadhani wenye fikra potofu na magaidi.

Share this:

Related Fatwas