Upande wa Kimaadili wa Hukumu Kivit...

Egypt's Dar Al-Ifta

Upande wa Kimaadili wa Hukumu Kivitendo katika Sharia ya Kiislamu.

Question

Upande wa Kimaadili wa Hukumu Kivitendo katika Sharia ya Kiislamu.

Answer

(Wema ndio Mfano)

Utafiti uliowasilishwa kwenye kikao cha tatu cha kazi za maarifa ya Kiimani katika mitazamo mbalimbali kuhusu:

(Sharia na Maadili)

Mkutano umefanyika katika mji wa Munister nchini Ujerumani

Kuanzia tarehe 3 – 5 November 2012.

Umeandaliwa na Chuo cha Kijerumani cha Tafiti za Kimashariki Beirut

Kwa ushirikiano na kituo cha tafiti za malezi ya kidini na imani ya Kiislamu Chuo Kikuu cha Munister.

Utafiti umewasilishwa Na:

Ahmad Mamduh Saad

Katibu wa Fatwa na Mkurugenzi Idara ya Tafiti za Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.

 

Maana ya Hukumu za Kisharia Kivitendo.

Hukumu kwa maana ya kilugha: Kuhukumu kitu kuwa kipo hivi au hakipo hivi ([1]).

Ama hukumu kwa maana ya Kisharia: Ni maelezo ya Mwenyezi Mungu yanayohusiana na vitendo vya waliopewa amri kwa kutakiwa au kuchagua au hali.

Maelezo: Ni kuelekeza maneno yenye faida kwa mwingine ambapo huyo mwingine atayasikia, na hapa kusudio ndio lake: Yanayoongelewa, nayo ni maneno yenye faida yanayoelekezwa kwa mtu mwingine, ni katika mlengo wa kutumia chanzo na kukusudia jina la mtendewa, neno maelezo limeongezwa Tamko Takatifu ili kuondolewa maneno ya wengine kwani hayazingatiwi hukumu.

Yanayohusu: Maana yake yanayofungamana, kuhusiana kunakuwa kabla ya kuwepo mpewa amri, au baada ya kuwepo kwake kabla ya kutumwa ujumbe. Na kunafikiwa baada ya kuwepo ujumbe.

Vitendo: Ni uwingi wa kitendo, na kusudio lake: Kinachofanywa na mpewa amri ikiwa ni kauli au kitendo au kuamini.

Wenye kupewa amri: Ni uwingi wa mtu aliyepewa mari, na kusudio lake: Ni mtu aliyebaleghe mwenye akili timamu ambaye amefikiwa na ujumbe.

Kutakiwa: Maana yake kutaka, ni sawa sawa kutakiwa kufanya kitendo au kuacha, lazima au si lazima, ndani yake kuna sehamu nne: Wajibu, Sunna, Haramu na Kuchukiza.

Hiyari: Ina maana kati ya kutenda au kuacha, nayo ni halali.

Tamko: Ni maelezo yaliyopo ya kitu kuwa sababu au sharti au kizuizi au usahihi au uharibifu, kwenye hivyo inakusanya kitendo cha mtu aliyepewa amri, kama vile uzinzi unalazimisha adhabu, na kutofanya kwake, au jua kupindukia sababu ya wajibu wa Swala ya adhuhuri, na kuharibu kusiko na lazima, kama vile ulevi sababu ya kulazimika uharibifu wa mali ya mwingine wakati wa kulewa kwake ([2]). 

Hukumu kivitendo: Inafungamana na kitendo cha mtu aliyebaleghe, kwa maana ya kutenda kwake, na kigezo hiki kinaondoa hukumu isiyo kivitendo, mfano wa hukumu za kielimu – nayo misingi ya dini – makusudio yake: Ni elimu tu, kwa maana kuamini kunakoegemea dalili na hukumu za kinadharia za Kisharia, kama vile elimu kuwa makubalianao ya Wanachuoni ni hoja ([3]).

%%%

Nafasi ya Maadili katika Sharia ya Kiislamu

Maadili mema ni uwingi wa neno maadili, na maadili ni tabia na mwenendo mzuri, nayo inaonesha wasifu wa nafsi na sura ya ndani ya mwanadamu, kama vile tabia zake za nje zinaonesha sura yake ya nje kwa upande wa uzuri au ubaya, hivyo tabia zake za nje zinaonesha pia sura yake ya ndani kwa namna iliyotajwa,

Mwanadamu ana sura mbili:

Sura ya Kwanza: Ni sura ya nje, nayo ni umbile lake ambalo Mwenyezi Mungu ameumba mwili wake, na sura hii ya nje miongoni mwazo ni: Uzuri na ubaya.

Sura ya Pili: Ni sura ya ndani, ambayo ndio umbile la nafsi imara thabiti inayofanya vitendo kwa wepesi bila ya kuhitaji fikra na mtazamo.

Asili hutumika kwa kila kinachompatia mwanadamu sifa ambazo zinakuwa kama tabia zake, nayo huitwa “Majukumu asili” lakini vile vile huitwa alivyoumbiwa mwanadamu miongoni mwa vitu asili, nayo huitwa “Hisia asilia”.

Miongoni mwa hayo: Ni pamoja na Hadithi iliyopokewa na Abu Daud katika Kitabu chake kauli ya Mtume S.A.W akimuambia Mundhir Al-Ashajj R.A:

“Hakika yako una sifa mbili anazipenda sana Mwenyezi Mungu: Sifa ya Akili na Upole, Mundhiri akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je nijipambe nazo sifa hizo au Mwenyezi Mungu amenijalia nazo. Mtume S.A.W akasema: Bali Mwenyezi Mungu amekujalia nazo. Mundhir akasema: Namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameniumbia sifa mbili anazozipenda Yeye na Mtume wake”.

Tabia inakusanya mambo mazuri na mabaya, kwa sababu hiyo hakuna mtu anayetenganisha aina mbili hizi kwa kutamka tu neno tabia, bali lazima abainishe, kwa mfano anasema: Tabia nzuri au tabia mbaya, lakini pindi ikiitwa bila kufungamanishwa humaanisha moja kwa moja ni tabia nzuri ([4]).

Kwa kuanza ni kuwa, hakuna fikra ya kidini bila ya kuwepo fikra ya kimaadili, kwani Sharia ya Kiislamu imekuja na maadili kupewa kipaombele na umuhimu mkubwa, ikaja na maandiko mengi kusifu tabia njema na na kuchukizwa na mwenye tabia mbaya, miongoni mwa hayo: Sharia haikuamrisha moja kwa moja kufikia tabia njema na kujipamba nayo, kwani amepokea Imamu Tirmidhy kutoka kwa Abi Dharri Al-Ghaffari R.A amesema: Mtume S.A.W aliniambia:

“Muogope Mwenyezi Mungu popote ulipo, na fuatilia ubaya kwa jema hulifuta, na uishi na watu kwa tabia njema”.

Vile vile Sharia ikazungumza kuwa miongoni mwa makusudio muhimu ya Ujumbe wa Mtume Muhammad ni pamoja na kukamilisha upande wa maadili mema, kwani imepokewa katika Sunna zake kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema: Mtume S.A.W amesema:  “Hakika nimeletwa ili kukamilisha tabia njema”, maana yake: Watu waliokuwa ndani ya zama za Utume wanatabia nyingi nzuri kutokana na yaliyobakia kwao miongoni mwa Sharia za Manabii wao, na walikuwa wamepotea kwa ukafiri wengi miongoni mwao, hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akamleta Mtume wake S.A.W ili kuja kukamilisha tabia njema, au Mtume S.A.W ameletwa akiwa amekusanya tabia njema zilizoachwa pamoja na kuongezewa zile zilizobaki ([5]).

Na Mtume alikuwa anamuomba Mola wake Mtukufu amruzuku tabia njema na amuondoshee tabia mbaya, imepokewa na Imamu Muslimu katika Sahihi yake kutoka kwa Ally Ibn Abi Twalib R.A kuwa Mtume S.A.W alikuwa pindi anaposwali husema: “….na uniongoze kwenya tabia njema hakuna muongozaji isipokuwa Wewe, na uniondoshee ubaya hakuna wa kuondoa isipokuwa Wewe”.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesifu tabia yake nzuri katika kauli yake:

{Na hakika wewe una tabia tukufu} Al-Qalam: 4. Pamesemwa: Tabia zake zimeitwa tabia tukufu, kwa kukutana pamoja na maadili mema ([6]).

Imepokewa na Imamu Ahmad katika kitabu chake kutoka kwa Saad Ibn Hishaam amesema: Nilimuuliza Bibi Aisha R.A nikasema: Nifahamishe kuhusu tabia za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W? akasema: “Tabia zake zilikuwa kama Qur`ani”, kwa maana: Kile kilichoelezewa na Qur`ani miongoni mwa yaliyomazuri na kuyasifia pamoja na kuyatolea wito Mtume S.A.W alikuwa amejipamba nayo, na kila kilichofanywa kibaya na Qur`ani na kukataza Mtume S.A.W alijitenga nacho na kuwa mbali nacho, hivyo Qur`ani ilikuwa ni kielelezo cha tabia zake, na kama vile maana ya Qur`ani haina mwisho basi hufahamika kuwa ukamilifu wa tabia zake hauna mwisho ([7]).

Sharia imebainisha kuwa tabia za mwanadamu kila uzuri unapoongezeka hilo linaendana na ongezeko la Imani yake na kukaribia ukamilifu, kwani imepokewa na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Waumini waliokamilika Imani ni wale wabora wao wa tabia”.

Imepokewa na Maruuzi katika kitabu cha “Taadhiim Qadra Swalaat” kwa tamko:

“Waumini wakamilifu wa Imani ni wale wabora wao wa tabia, hakika mtu kuwa Muumini na katika tabia zake akawa na kitu kinachompunguzia Imani yake”.

Hadithi zimejirudia sehemu nyingi kusisitiza wasifu wa tabia njema, kwani imepokewa na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Nuwas Ibn Sam’an R.A amesema: Nilimuuliza Mtume S.A.W kuhusu wema na dhambi, akasema:

“Wema ni tabia njema, na dhambi ni kile kinachozunguka kifua chako na ukachukia watu kukijua”.

Imepokewa na Abu Daud katika Kitabu chake kutoka kwa Bibi Aisha R.A amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W anasema:

“Hakika Muumini kwa tabia yake njema hufikia daraja ya mfungaji na mwenye kusimama usiku kufanya ibada”.

Imepokewa na Al-Hakim katika kitabu cha Mustadraku kutoka kwa Usama Ibn Sharik R.A amesema: Tulikuwa tumekaa mbele ya Mtume S.A.W kana kwamba kwenye vichwa vyetu kuna ndege, hakuna miongoni mwetu mwenye kuzungumza, mara wakaja mabedui wakauliza: “…..Ni mja gani anayependwa sana na Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni yule mwenye tabia nzuri”.

Imepokewa na Imamu Bukhary katika Sahihi yake kutoka kwa Abdillah Ibn Amr R.A kuwa Mtume S.A.W alikuwa anasema: “Hakika mbora wenu ni mwenye tabia njema”.

Imepokewa Hadithi pia na Al-Baihaqy katika Kitabu chake kutoka kwa Abi Thaalaba Al-Khashny R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: 

“Hakika mtu mwenye kupendwa zaidi kwangu na yupo karibu zaidi na mimi ni yule mbora wenu wa tabia, na mtu mwenye kuchukiwa zaidi kwangu na kuwa mbali zaidi na mimi ni yule mbaya wenu wa tabia”.

Na Hadithi nyingine imepokewa na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Abi Dardai R.A amesema: Nilimsikia Mtume S.A.W anasema:

“Hakuna kitu kinachowekwa katika mizani kizito zaidi ya tabia njema”.

Na imepokewa pia kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema: Siku moja Mtume S.A.W aliulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu wengi Peponi, akasema: Ucha-Mungu na tabia njema”.

Imepokewa na Al-Maruzy katika kutukuza nafasi ya Swala kuna mtu mmoja alikuja mbele ya Mtume S.A.W akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni matendo gani yaliyobora zaidi? Akasema: “Tabia njema” kisha akaja upande wa kushoto kwake na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni matendo gani yaliyobora zaidi? Akasema: “Tabia njema”.

Imepokewa pia na Ahmad katika Musnadi yake kutoka kwa Raafii Ibn Makith R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Tabia njema huongeza kheiri, na tabia mbaya huondoa kheiri”.

Imepokewa pia na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Abi Said Al-Khudry R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Mambo mawili hayakutani pamoja kwa Muumini: Ubahili na tabia mbaya”.

Hadithi nyingine imepokewa na Al-Kharaitwi katika “Tabia njema” kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Miongoni mwa ubaya wa mwanadamu ni tabia mbaya”.

Mtume S.A.W amebainisha kuwa mtu asiyejipamba na tabia njema basi Imani yake na dini yake vinafikwa na upungufu na kuto kamilika, mpaka ameelezea kukataa Imani, kwani imepokewa na Ahmad katika Musnadi yake kutoka kwa Anas Ibn Maliki R.A amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alihutubia na kusema: “Hakuna Imani kwa mtu asiye na uaminifu, wala hana Imani mtu asiyetekeleza makubaliano”.

Maelezo katika maana hii ni mengi sana, ambalo tunamaanisha ni kuwa tabia njema sio sehemu ya mfumo wa Uislamu bali Sharia Takatifu na Dini vyote ni ibara ya tabia njema, na maadili mema ndio sura ya Uislamu na roho yake inayotembea pande zake zote, na mwenye kumzidi ndugu yake katika tabia njema kwa hakika atakuwa amemzidi katika Dini.  Abu Al-Atahiya amesema vizuri pale aliposema:

Hakuna dunia bila ya dini – na maadili mema ([8]).

%%%

Njia za Kufahamu Hukumu Kimaadili katika Sharia ya Kiislamu

Imeelezwa kwenye maelezo yaliyopita kuwa maadili mema ni katika jumla ya mambo yanayohitajika Kisharia, na kuzungukwa kati ya jambo la lazima au jambo linalohitajika, ulazima na kuhitajika ni katika maelezo ya Sharia, wala hayaelezwi isipokuwa katika Sharia, kwa kutumia akili tu haiwezi kufahamu jema au baya, kwani jema ni lile liloonekana na Sharia jema, na baya ni lile liloonekana na Sharia kuwa ni baya, hivyo wema na ubaya ni Sharia mbili na wala si mambo mawili ya kiakili.

Masuala ya wema na ubaya ni maneno maarufu yamefanyiwa tafiti nyingi na Waislamu wazungumzaji wa madhehebu mbalimbali na kupishana uelewa wao, lakini uelewa wa watu wa haki ni kuwa. wema na ubaya sio sifa binafsi za wema na ubaya, na wala hayo si yenye kufahamika na akili tu au mtazamo, bali huitwa tu kwa tamko la wema na ubaya kunakuwa kwa mazingatio yasiyo ya kweli, bali ni nyongeza inayowezekana kubadilishwa kwa kuangalia watu wakati na hali, kwa mfano vitendo vikiwa vinagawanyika katika kukubalina na lengo – ambalo ni wema – na kutofautiana na lengo  – ambalo ubaya – na kwenye kutokubaliana wala kutofautiana – nako ni uovu – mazingatio haya yanaweza kuwa kitendo kimoja chema kwa upande unaokubaliana lengo lake, na uovu kwa upande wa aliyekinyume na lengo lake, kama vile kwa mfano kumuua Mfalme, kitendo hicho ni kibaya na kiovu kwa upande wa wafuasi wake, lakini ni kitendo chema kwa upande wa maadui zake, hivyo ni jambo la ziada si la kujitegemea, na hilo sio sawa na weusi na weupe kwa mfano, kwani haiwezi kuonekana sehemu nyeusi ni nyeupe kwa upande wa watu wawili ([9]).

Imamu Fakhru Diin Ar-Razy pamoja na wafuasi wake walifuata njia waliyofupisha mvutano wakasema: Wema na ubaya huitwa kwa maana tatu: Maana ya Kwanza: NI inayoendana na asili kama vile tamu na chungu furaha na huzuni, hili halina mvutano kwa sababu ya kutofautiana malengo. Maana ya Pili: Kitu kuwa na sifa ya ukamilifu au upungufu, kama vile elimu na ujinga, ambavyo kwa maana hizi mbili ni za kiakili, kwa maana: Hufahamika kwa akili. Maana ya Tatu: Kitendo kuwa cha wajibu wa kupata thawabu adhabu sifa na ubaya, hii ni sehemu ya mvutano, na mvutano ni kitendo kuwa kinaendana na ubaya hivi sasa na adhabu hapo baadaye ([10]).

Katika haya Wanachuoni wa taaluma ya Misingi ya dini katika maelezo yao kuhusu hakimu ambaye ni moja ya nguzo ya hukumu ya Kisharia: “Hakimu ni Mwenyezi Mungu” ([11]), na katika maana yake: “Haifikiwi hukumu isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu” ([12]), na katika maana hizo mbili: “Hakimu ni Sharia na wala si akili” ([13]). 

Pindi yanapoelezwa haya basi hukumu kimaadili katika Sharia ya Kiislamu hufahamika kwa vyanzo hivyo hivyo na dalili ambazo hufahamika hukumu zingine za Kisharia, vyanzo vilivyokubaliwa ni vinne, navyo ni: Qur`ani Tukufu. Sunna Takatifu. Ijmaai na Al-Qiyaas. Na yafuatayo ni maelezo ya kila kimoja:

Kwanza: Qur`ani.

Ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoteremshwa kwa Mtume S.A.W ili kuwa muujiza unaonesha Yeye ni Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kushindwa kuletwa angalau sura ya mfano wake, kisomo chake ni ibada, nayo imeandikwa katika Msahafu, iliyoanza kwa Suratul-Fatiha, na kuhitimishwa na Suratul-Naas, iliyoletwa kwetu kwa mapokezi ya wengi kwa kuandikwa na kusomwa kizazi na kizazi, iliyolindwa na kuingizwa mabadiliko yeyote au kubadilishwa ([14]).

Qur`ani Tukufu kwa mtazamo wa Waislamu ni Maneno ya Mwenyezi Mungu, hivyo yenyewe inaeleza utashi wa Mungu, na Qur`ani Tukufu imekuja na aina nyingi za hukumu:

Aina ya Kwanza: Hukumu za Kiimani: Zinahusu yaliyowajibu kwa mtu aliyebaleghe kuamini Mwenyezi Mungu Malaika wake Vitabu vyake Mitume wake na siku ya Mwisho.

Aina ya Pili: Hukumu za Kimaadili: Zinahusiana na wajibu kwa mtu baleghe kujipamba na tabia njema na kujiondoa na tabia chafu.

Aina ya Tatu:  Hukumu ya vitendo: Inahusiana na yanayotoka kwa mtu baleghe miongoni mwa maneno vitendo na makubaliano ([15]).    

Pili: Sunna.

Ni yaliyokuja kutoka kwa Mtume S.A.W miongoni mwa kauli au kitendo au kukubali.

Sunna inazingatiwa ni ufafanuzi wa Qur`ani Tukufu, na yaliyokuwa katika aina hizi kwa upande wa Sharia, na kuletwa kwetu kwa upokezi sahihi basi inakuwa ni chanzo kinachozingatiwa cha hukumu za Kisharia, na Qur`ani Tukufu yenyewe imewataka Waumini wamtii Mtume S.A.W na kumtii kwake kumeambatanishwa na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, pale Mola Mtukufu Aliposema: 

{Mwenye kumtii Mtume basi amemtii Mwenyezi Mungu} An-Nisaa: 80. Na akasema: {Na anacho kupeni Mtume chukueni} Al Hashri: 7.

Tatu: Ijmaa.

Nayo ni makubaliano ya wenyekujitahidi katika Umma wa – Kiislamu – baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad S.A.W ([16]).

Pindi inapofikiwa nguzo ya Ijmaa ndani ya zama za baada ya kufariki Mtume S.A.W wote waliomo kwenye zama hiyo miongoni mwa wenyekujitahidi Waislamu, na rai zao zote zikakubaliana juu ya hukumu moja katika masuala maalumu, hukumu hii iliyokubalika inakuwa haifai kwenda nayo kinyume, na wala haikubali kufanyiwa jitihada kwa mara nyingine na wenyekujitahidi wa zama zingine inayofuata baada ya zama yao.

Dalili ya hoja ya Ijimaa: Ni Hadithi iliyopokewa na Ibn Omar R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Hakika Mwenyezi Mungu haukutanishi Umma wangu – au alisema: Ummati Muhammad S.A.W kwenye upotofu, na uungaji mkono wa Mwenyezi Mungu upo kwa wengi, na mwenye kuwa peke yake ataingia motoni”.

Nne: Al-Qiyaas:

Nayo ni kukutana tukio lisilo na andiko la hukumu yake na tukio lenye andiko la hukumu yake kwenye hakumu ambayo ina andiko ili yawe sawa matukio mawili katika sababu ya hukumu hii.

Nguzo za Qiyaas ni nne: Asili – kinacholinganishwa nacho – tawi – kilinganishi – sababu shirikishi yenye kukusanya kati ya asili tawi na hukumu.

Ikiwa andiko linaonesha hukumu, na ikafahamika sababu ya hukumu hii kwa njia ambayo hufahamika sababu ya hukumu, kisha likapatikana tukio lingine linafanana na uhalisia wa andiko kwa kufikiwa sababu ya hukumu, hiyo ni sawa na uhalisia wa andiko katika hukumu kutokana na kuwa sawa katika sababu, kwa sababu hukumu inapatikana kwa kupatikana sababu ([17]).

Imekuja katika Sunna Takatifu kuwa Mtume S.A.W aliwahi kutumia Qiyaas katika kuleta dalili ya hukumu za matukio mengi ambayo yaliletwa kwake na hayakuwa na ufunuo kwenye hukumu zake, na wala hakukuwa na dalili maalumu ya hilo. Mtume kwa Waislamu ni kigezo.

Dalili hizi tatu za mwisho ukweli wa mapokeo yake ni Qur`ani Tukufu. Mola Amesema: {Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu} An-Nahl: 89. Imamu An-Nasafi amesema katika kutafasiri kwake:  {Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha} kinachofikisha {Kila kitu} katika mambo ya dini. Ama katika hukumu zilizotamkwa zipo wazi, vile vile katika yaliyothibiti kwa Sunna au Ijmaa au kwa kauli za Swahaba au kwa Qiyaas, kwa sababu marejeo ya yote ni Kitabu, ambapo kimeamrisha kumfuata Mtume wake S.A.W na kumtii kwa kauli yake:

{Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume} na kutuhimiza kujumuika kwenye Kitabu kwa kauli yake: {Na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini} kwa hakika Mtume S.A.W ameridhia kwa Umma wake kuwafuata Maswahaba wake kwa kauli yake: “Maswahaba wangu ni kama nyota yeyote mtakayemfuata mtaongoka” ([18]). Wamefanya jitihada wakafanya Qiyaas na wakafuata njia za jitihada na Qiyaas, pamoja na kuwa tumeamrishwa hilo kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Basi zingatieni enye watu wenye maono} ikawa Sunna Ijmaa kauli za Maswahaba na Qiyaas ni ufafanuzi wa Qur`ani, na ikabainisha kuwa imekuwa ni ufafanuzi wa kila kitu ([19]).

Sisi hata tukienda kina kiasi gani katika makundi mbalimbali ya fikra za Sharia ya Kiislamu ukweli wake utaendelea kuwa thabiti haukubali mjadala, nao ni kuwa lengo la mwisho nyuma ya kila juhudi za Wanachuoni ni kufikia kwenye chanzo pekee ambacho watu wote wanapaswa kunywea kwa ukaribu au kwa mbali: Hukumu ya Mwenyezi Mungu, nayo ni hukumu ambayo kwa sehemu ya kwanza imeandikwa na Qur`ani moja kwa moja, kisha inakuja Hadithi ili kufafanua na kuainisha, ikiwa hukumu haijapokewa ndani ya Qur`ani au Sunna basi Qiyaas huwa inajaribu kuielezea hukumu hiyo katika undani wake na uelewa wake wa kina, mwisho inakuja nafasi ya Ijmaa ikiwa jaribio la kufahamu hukumu hii katika ujumla wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake ndio ruhusa ya Sharia, na wala si wengine zaidi waamuzi wa amri yake kwa njia ya moja kwa moja au si ya moja kwa moja ([20]).

%%%

Fikra ya Maadili katika Urithi wa Kiislamu

Wanachuoni Waislamu wametoa mchango mkubwa katika asili ya fikra ya maadili kwa ujumla, miongoni mwa sura ya hilo ni katika urithi wa maandishi: Ni ngumu kuhesabu vitabu vingi vya aina mbalimbali, maelezo kuhusu fikra ya maadili yamekuwa baada ya zama za Mtume S.A.W ndani ya zama za Maswahaba wake Watukufu kisha zama za watu wa Taabiina na waliofuata baada yao, kisha zama za Maimamu waliofuata, yaliweza kufikishwa kwetu kupitia mwenendo wao na upokezi wa maneno yao, mwenye kupitia mfano wa kitabu cha “Hulyatu Al-Auliyaa” cha Abi Naeem Al-Aswabahaii kilichochapishwa vitabu kumi ataona mengi ya haya, kazi za utungaji vitabu ilikuwa haishamili sana kama ilivyotokea katika zama iliyofuata, lakini vitabu vilivyoandikwa mapema kwa upande huu vilianza kwa jina la: “Kitabu Az-Zuhdi” katika maudhui hii Wanachuoni wengi walitunga vitabu, mfano kama Abdillah Ibn Al-Mubaraka amefariki mwaka 181H, Wakii Ibn Al-Jarrah amefariki mwaka 196H, Ahmad Ibn Hanbal amefariki mwaka 241H na Hanad Ibn As-Sariyy amefariki mwaka 243H, huenda kitabu cha zamani zaidi ni “Kitabu Az-Zuhdi” cha Zaidi Ibn Qudama Abi As-Swalti Al-Kuufi amefariki mwaka 160H. Kisha vikafuata baada ya hapo mamia ya vitabu, mfano wa vitabu vya Al-Harith Al-Muhasaby, Abi Twalib Al-Makky, Ibn Abi Ad-Dunia, Al-Hakiim At-Tirmidhy, Al-Kharaitwi, Ibn Hazmi, Al-Mawrudy, Al-Baihaqy, Ar-Raghib Al-Aswfahany, Abi Hamid Al-Ghazaly, Ibn Jawzy, Ibn Qayyim na wengine mpaka zama zetu hizi ambapo ni ngumu kuwahesabu.

 Watunzi wa vitabu hivi wana maudhui mbalimbali, miongoni mwao wapo waliojikita zaidi pande za kiasili na kimtazamo, wengine waliangalia zaidi pande za maadili tabia na vitendo, na wengine walichanganya kati ya pande mbili.

Mfumo huu wa utungaji ulijikita na utafiti kuhusu siri za ibada, au maana za maadili katika hukumu za Kisharia, katika hilo Hakimu Tirmidhy aliyefariki mwaka 320H, aliandika katika kitabu chake cha “Al-Akbaas wal-Mughtariin”, na Abu Twalib Al-Makkiy alifariki mwaka 386H aliandika kitabu “Quutil-Quluubi”, Hoja ya Uislamu Al-Ghazaly amefariki mwaka 505H aliandika kitabu chake “Ihyaau Uluumi Diin” ambacho alikigawa milango minne, mlango wa Ibada, mashirikiano, yanayoangamiza na yanayookoa, vile vile Shaha Waliyyullah Ad-Dahlawi amefariki mwaka 1176H kitabu chake “Hujjatullah Al-Baaligha” na Sheikh Ahmad Al-Alawy aliandika kitabu kwa mfumo wa Kisufi katika Fiqhi ya Imamu Maliki jina lake: “Al-Manhul-Qudusiyya fii sherhi Al-Murshidy”, na Sheikh Mustafa Yussuf Salaam As-Shaadhily aliandika kitabu chengine kwa matini ya Abi Shujaa katika Fiqhi ya madhehebu ya Imamu Shaafi jina lake: “Jawaahiri Al-Itwlaai wa Duuru Al-Intifaa”, maana hii tunaikuta pia katika tafasiri ya Imamu Abu Qassim Al-Qushairy amefariki mwaka 465H kinachoitwa “Latwaaifu Al-Ishaarat”, vile vile katika tafasiri ya Imamu Fakhru Diin Ar-Raazy amefariki mwaka 606H, pia vitabu vingi vya Imamu Abdulwahab Asharany amefariki mwaka 973H, na kwa upande huo pia kitabu cha “Dhariia ilaa Makaarim Sharia” cha Raaghib Al-Aswfahany alifariki mwaka 502H, pia kitabu cha “Hikmatu Tashrii wa Falsafatuh” cha Sheikh Ally Al-Jarjawy amefariki mwaka 1340H- 1922, na Sayyid Muhamma Muhammad Swadiq As-Swadri miongoni mwa Wanachuoni wa hivi karibuni wa Imaamia, amefariki mwaka 1999 ameacha kitabu muhimu sana jina lake: “Fiqhul-Akhlaq” kimechapwa juzuu mbili, amezungumzia humo mahusiano kati ya Fiqhi na Maadili, akiielezea kupitia milango mbalimbali ya Fiqhi.

Vitabu hivi na mfano wake havijaishia kwenye maandishi ya Fiqhi ya kawaida kwa kueleza tu masharti nguzo wajibu yanayoharibu na mfano wake, bali imeeleza hayo na kuzama zaidi kwenye siri na hukumu za uanzishaji wa hukumu na kuonesha pande zake za kimaadili na kiroho, Sheikh wetu Mwanachuoni Mtukufu Dr. Ally Juma Mufti wa Misri – Mwenyezi Mungu amuhifadhi - ana mihadhara mingi aliyoitoa katika Chuo cha Masomo ya juu ya Kiislamu Kiarabu na Sayansi ya Kisufi kinachomilikiwa na Academy ya Al-Ashiiratul-Muhammadia Jijini Cairo kuhusu Fiqhi ya Kisufi ya hukumu za Kisharia, akaweka msingi wa maana hizi na kuzungumzia, iliandikwa na kuchapwa na baadhi ya wanaompenda kwa jina la: “Muhadharat fii Fiqhi Suuf li Ahkaami Sharia”.

Huenda tunachokizungumzia ni maadili ya wema katika hukumu za Kisharia ndio yameambatana zaidi na muelekeo wa hivi karibuni kuliko jambo jingine, kwa sababu mwanadamu lau ataona yanayoletwa na vitendo pamoja na maneno basi atakuwa amefahamu siri kubwa katika siri za Sharia, jambo linalozalisha kwake nguvu ya yakini na kuongeza Imani na hivyo kuwa mtu mwema mwenye kunufaisha nafsi yake na ulimwengu unaomzunguka.

%%%

Wema Maana yake na Nafasi yake katika Sharia ya Kiislamu

Maana ya Wema:

Maana ya wema kwa upande wa lugha ni kinyume cha ubaya ([21]), kwa mfano tunasema: Umefanya wema kwenye jambo hili, kwa maana umefanya kitendo kizuri kwa umakini na uzuri.

Ama maana yake kimsamiati husemwa maana mbili: Maana ya Kwanza: Kuneemesha mwingine, husemwa kwa mfano: Fulani amenifanyia wema. Maana ya Pili: Kufanya wema katika kitendo chake, na hilo pindi anapomfundisha elimu njema, au kufanya kitendo chema ([22]).

Tofauti kati ya wema na neema: Wema ni mpana zaidi, kwa sababu unakuwa kwa mtu mwenyewe na kwa mwingine, lakini neema haiwi isipokuwa kwa kumfanyia mwingine ([23]).

Nafasi ya wema:

Wema una daraja na viwango, daraja yake ya juu ni ule unaofanywa na mja kwa Mola wake, na kila mja anapoufikia wema kwa upande huu ndio wema unapokuwa umejikita na kujidhatiti zaidi ya viwango vyengine, kama vile kuifanyia wema nafsi yake na mwingine, imepokewa na Imamu Bukhary na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema, pindi Malaika Jibril alipomuuliza Mtume S.A.W kuhusu wema akasema: “Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama kwamba unamuona, ikiwa wewe humuoni basi Yeye anakuona”. Huu ndio msingi wa wema na ukamilifu wake, na kwa msingi huu hurejea misingi iliyobaki na matendo yanayohitajika kutendwa na watu waliopewa amri.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio Mwema zaidi kwa waja wake, kwanza amewafanyia wema kwa kuwaweka ulimwenguni, kwani Mola Mtukufu amesema: {Je! Hakumbuki mwanadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?} Mariam: 67. Na akafanya umbile lao lenye hekima ya hali ya juu. Mola Mtukufu akasema: {Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji} Al-Muuminun: 14.

Kisha akawafanyia wema wa pili kwa kuwaongezea, na akawaneemesha kwa neema zisizohesabika na uaminifu wake hauna idadi. Mola Mtukufu Amesema:

{Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamuwezi kuzidhibiti} Ibrahim: 34.

Kujipamba na tabia njema ni mja kujipamba na tabia za Mwenyezi Mungu, ukamilifu wa hali ya mja hauwi isipokuwa kwa kujipamba na tabia za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ukamilifu wa Manabii ulikuwa katika kujipamba kwao na tabia za Mwenyezi Mungu.

Na katika tafasiri ya kauli ya Mama wa Waumini Bibi Aisha R.A katika wasifu wa Mtume wetu Muhammad S.A.W: “Tabia zake zilikuwa kama Qur`ani” Imamu Al-Marswafy amesema: “Amekusudia katika kauli yake “Tabia zake zilikuwa kama Qurani” ni kule kujipamba kwake na tabia za Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini hakusema hivyo kwa heshima” ([24]).

Imamu Al-Ghazaly amesema: Ukamilifu wa mja na furaha yake ni katika kujipamba na tabia za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujipamba kwa maana ya sifa zake na majina yake kwa kiasi cha anachofikiria kwake….na….kufanya juhudi inayowezekana kufikia sifa hizo na kujipamba nazo pamoja na kujipamba na mazuri yake, na kwa kiwango hicho mja anakuwa mcha-Mungu, kwa maana ya kuwa karibu na Mola Mtukufu, anakuwa rafiki wa Malaika, kwani wao wapo karibu zaidi, hivyo yeyote mwenye kupiga hatua moja kufikia sifa zao hupata kitu cha ukaribu wao, kwa kiwango cha aliyepata kutokana na sifa zao ukaribu wao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ([25]).

Ibn Qayyim amesema: “Mwenye kufungamana na sifa katika sifa za Mola Mtukufu sifa hizo zitamuingiza kwake na kumuunganisha….. na pamesemwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa ufunuo Nabii Daud akimuambia: “Jiveshe tabia zangu, kwani miongoni mwa tabia zangu ni Mimi Mwingi wa subira”, na Mwneyezi Mungu Mtukufu anapenda majina yake na sifa zake, na anapenda kwa mujibu wa sifa zake kuonekana athari zake kwa mja, kwani Yeye Mwenyezi Mungu ni mzuri na anapenda mazuri, Msamehevu anawapenda watu wenye kusamehe, Karimu anawapenda watu wenye ukarimu, Mwingi wa elimu anawapenda watu wenye elimu, Mwingi wa kusubiri anapenda wenye kusubiri, Yeye ni Witiri anapenda watu wa witiri, ni Mwenye nguvu, na Muumini mwenye nguvu anapendwa zaidi na Yeye kuliko Muumini mnyonge, Mwingi wa shukrani anawapende wenye kushukuru, na ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda wenye kusifika kwa sifa zake basi Yeye yu pamoja nao sawa na sehemu yao katika wasifu huo ([26]).

Na kwa upande wa tabia ya wema: Sheikh Ezz Diin Ibn Abdilsalaam anasema: “Hiafai kuongoza dini kwa mtu asiyejipamba na adabu za Qur`ani wala kujipamba na sifa za Mwenyezi Mungu kwa kadiri awezavyo” ([27]), kisha akasema: “Somo katika kujipamba na sifa ya wema uzuri neema na mambo mazuri”. Akasema: Uzuri neema na mambo mazuri ni katika jumla ya wema, kwani wema unaelezea upande wa manufaa yote au kuondoa madhara kwa ujumla, basi fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyofanya wema kwako, na neemesha kama Mwenyezi Mungu alivyokuneemesha, ni wajibu kuwa na sifa nzuri, subira nzuri, wema mwingi, kujipamba na tabia ya Mfalme Mtukufu, wala usisahau mambo mazuri, kwani Mola wako Amesema:  {Wala msisahau mambo mazuri kati yenu} Al-Baqarah: 237, muunge aliyekukata undugu, mpe aliyekunyima, msamehe aliyekudhulumu, subiri kwa aliyekutukana, na fanya wema kwa aliyekufanyia ubaya” ([28]).

Sharia Tukufu imeangalia uwazi wa mtazamo wa waliopewa amri umuhimu wa tabia ya wema na ukubwa wake, ndipo ikaja amri katika maandiko ya Kisharia, miongoni mwa amri hizo kauli ya Mola Mtukufu: إِ {Hakika Mwenyezi Mungu ana amrisha kufanya uadilifu na hisani} An-Nahli: 90. Na kauli yake: {Na fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wewe wema} Al-Qasas: 77.

Na mwisho wa wema na malipo ya wafanya wema: Mola Mtukufu Amesema:

{Hakika Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wenye kumcha na watendao mema} An-Nahli: 128.

Na Akasema tena: {Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema} Al-Baqarah: 195.

Na Amesema: {Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema} Al-Aaraf: 56.

Na Akasema tena: {Hakika Sisi hatupotezi malipo ya anaye tenda mema} Al-Kahfi: 30.

Mola Amesema pia: {Ati yaweza kuwa malipo ya wema ni wema?} Ar-Rahman: 60.

Imapokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Shadad Ibn Aus R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameandika wema kwenye kila kitu” maana yake: Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya wema juu ya kila kitu au ndani ya kila kitu, au amefanya wema katika usimamizi wa kila kitu ([29]), wala hakuna tofauti katika hili kati ya Muislamu na Muislamu, wala kati ya mwanadamu mwenye akili na mnyama asiye na akili, wala kati ya mtu aliye hai na aliyekufa au vitu visivyo na uhai, kwani ni lazima kushirikiana kwa wema na vitu vyote vya ulimwengu, na kabla ya ulimwengu na Mtengeneza wa ulimwengu, tamko “Kila” ni katika muundo wa ujumla, nao ni ujumla wenye nguvu zaidi katika kuelezea ([30]), mpaka ikasemwa: Hakuna baada yake katika maneno ya Waarabu neno la jumla zaidi ya hili ([31]).

Sunna za Mtume S.A.W zimefikia uangalizi wa juu wa wema mpaka kufikia Hadithi zilizopokewa pasi ya kujirudia kiasi cha Hadithi mia na hamsini, ama zilizopokewa kwa maneno yenye uhusiano na maudhui ni nyingi zaidi, katika uwingi huu ambao uliotawala katika Sunna ni dalili juu ya umuhimu wa wema na ukubwa wa nafasi yake ([32]).

Maandiko haya yaliyotajwa ni sehemu ya maandiko ambayo yanazungumzia wema kwa ujumla wake, na maandiko yaliyozungumzia wazi sehemu ya wema ni mengi mno ([33]).

Mwenye kuzingatia maandiko hayo yatambainikia kuwa wema ni moja ya mihimili muhimu ambayo dini ya Uislamu inazunguka kwenye muhimili huo, na yenyewe inaeneza wema kwa mtu mwinyewe kwa ndugu yake mwanadamu bali na kwa wengine miongoni mwa viumbe vya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuanzia wanyama mpaka wema wa mwanadamu kwa vitu visivyo na uhai na ulimwengu kwa ujumla kwa kaenea dalili, nayo inafahamika kutokana na mwenendo wa Mtume S.A.W pamoja na mwenendo wa Maswahaba wake Watukufu na waliowafuata kwa wema na wenye kufuata mwenendo wao na kufuata uongovu wao miongoni mwa Wanachuoni wa Umma huu na waja wema.

Na mwenye kufuata mgawanyiko wa Sharia katika milango yake yote atagundua kuwa wema maana yake kuu kimaudhui inayolazimika nayo bila ya kuachana, na hukumu zake zinapita kama maji yanavyopita katika maua, maelezo ni marefu juu ya kadhia hii na mwenendo wa Sharia na hukumu zake umeelezewa na Imamu Ezz Diin Ibn Abdilsalaam aliyefariki mwaka 660H katika kitabu chake cha ajabu na cha aina yake alichokiita: Shajaratul-Maarifi wa Ahwaal wa Swaaleh Al-Aqwaal wal- Aamaal”.

Na maelezo yafuatayo tunaleta hukumu za Kisharia za vitendo katika milango ya Fiqhi mbalimbali na zingine, na tunaelezea yaliyomo miongoni mwa maana za wema jambo linalosisitiza tuliyoyasema na kuyathibitisha akilini, na hukumu hizi zilizonyingi na chache katika nyingi, na makusudio ni kuleta mifano na wala si makusudio kuleta idadi.

Wema katika Hukumu za Vitendo za Sharia

Ibada:

Usafi.

Sharia Tukufu imetoa umuhimu mkubwa kwenye usafi na kuelezea umuhimu wake na kuwasifu watu wake, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha} Al-Baqarah: 222.

Na Imamu Muslimu amepokea Hadithi kutoka kwa Abi Maliki Al-Ash’ari R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Usafi ni sehemu ya Imani”.

Tabia ya wema imeonekana sehemu nyingi katika hukumu zinazohusu mlango huu miongoni mwake:

Uharamu wa kukojoa kwenye maji yasiyotembea, imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Jabiri Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amekataza kukojoa kwenye maji yasiyotembea, na hekima ya hilo ni kuwa kitendo hiki kinachafua maji na kuyanajisi pamoja na kuyaharibu kwa matumizi ya watu wengine, hivyo hao wengine hawataweza kunufaika nayo kwa kunywa au kujisafishia au kwa matumizi mengine.

Kuhitajika kiuchumi kutumia maji katika kujisafisha, na kuchukiza kuyatumia hovyo, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Anas R.A kuwa amesema: “Mtume S.A.W alikuwa anaoga kwa kutumia pishi moja ya maji mpaka vibaba vitano, na akitawadha hutumia kibaba kimoja”. Na kibaba ni kiasi cha kujaza maji kwenye viganja viwili vya mikononi bila kuvifunika wala kuvukunjua sana. Na pishi ni vibaba vinne ([34]).

Imepokewa Hadithi na Ibn Maja kutoka kwa Abdillah Ibn Amr R.A kuwa Mtume S.A.W aliwahi kupita kwa Saad Ibn Abi Wiqaas R.A naye akiwa anatawadha, akasema: “Ni matumizi gani haya mabaya ya maji? Akasema: Kwani kwenye kutawadha kuna matumizi mabaya? Akasema: Ndio: Hata ukiwa kwenye mto wenye maji yanayotembea”.

Swala:

Sharia imehimiza na kupendezesha swala ya jamaa kwa maana Swala ya pamoja, na akaifanya kuwa na ubora mkubwa, kwani imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Mtu kuswali kwake Swala ya jamaa huizidi Swala yake ya nyumbani kwake na kuswali kwake sokoni kwa daraja ishirini na saba”.

Pamoja na upendezeshaji huu Maimamu wameamrishwa kuwafanyia wepesi wenye kuswali, kwani inachukiza kwa Imamu kuwarefushia watu Swala yao bila ya ruhusa yao, kwani Imamu Muslimu amepokea Hadithi kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Mmoja wenu anaposwalisha watu basi na afanye wepesi, kwani miongoni mwao wapo watoto wadogo, watu wazima, watu dhaifu na wagonjwa, pindi anaposwali peke yake basi na aswali atakavyo”.

Funga:

Miongoni mwa makusudio ya funga na siri zake ni kuwaiga Malaika katika kuzuia matamanio kadiri inavyowezekana kwani wao wameepukana na matamanio, na mwanadamu daraja yake ni zaidi ya daraja za wanyama, kwa uwezo wake kwa kutumia nuru ya akili kuvunja matamanio yake, na chini ya daraja za Malaika kwa udhibiti wa matamanio na kuwa kwake anafanyiwa mitihani kwa kupambana kwake, kila anapozama kwenye matamanio hushuka chini ya waliochini na kuzidiwa na wanyama, na kila anapobana matamanio yake hupanda daraja za juu ya waliyo juu na kufikia daraja za juu ya daraja za Malaika, na Malaika ni waja waliokaribu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ambaye huwaiga Malaika na kujifananisha nao kwa tabia zao hujiweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu kama vile ukaribu wao, kwani kujifananisha na ukaribu ni kuwa karibu, wala si ukaribu kwa sehemu bali kwa sifa ([35]).

Na maana ya wema huonekana pia katika hukumu nyingi za funga, miongoni mwazo:

Kama vile Sharia Takatifu imehimiza funga, kwani imewaongoza waliamrishwa kufunga kusudio si kujizuia na kula kunywa na kuingilia tu bali yenyewe ni shule ya kuifunza nafsi mambo mema na kuipa mazoezi ya kusubiri kutokana na matamanio, na kudhibiti hasira kwenye nafsi ya mwanadamu, kwani imepokewa Hadithi na Imamu Bukhari pamoja na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Funga ni kinga mwenye kufunga hapaswi kuongea maneno machafu wala ya kijinga, ikiwa mtu amempiga au kumtukana basi na aseme mara mbili: Mimi nimefunga”.

Maana ya kinga: Kwa maana ya ulinzi na sitara, kwani yenyewe humkinga mfungaji na vitendo vya maasi duniani, ikiwa ndio hivyo, basi huko Akhera anakuwa na kinga ya moto, na kusudio la maneno machafu: Ni maneno mabaya, na kauli yake: Wala asifanya ujinga: Kwa maana, asifanye kitu katika vitendo vya watu wajinga, kama vile kupiga kelele kufanya mambo ya kipumbavu na mfano wake, wala haifahamiki katika haya kuwa ibada isiyokuwa ya funga inahalalisha yaliyotajwa bali kusudio ni kuwa kuzuia hayo kunapatikana kwenye funga ([36]).

Sheria imependezesha wema kwa wafungaji, kwa kuwafanyia wema na kuwatosheleza chakula cha kufuturu kwao,kwani imepokewa na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Zaidi Ibn Khalid Al-Jahny R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Mwenye kumfuturisha mfungani, anakuwa na malipo mfano wa malipo ya mfungaji, pasi ya kupungua chochote katika malipo ya mfungaji”.

%%%

Zaka na Sadaka:

Sharia Takatifu imehimiza kutoa mali inayopendwa sana na nafsi na kuwapa watu masikini na wanaostahiki zaka na sadaka. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda} Aal-Imran: 92. Kwa maana hamtoufikia wema wa kweli ambao ni ukamilishi wa kheir, au hamtaufikia wema wa Mwenyezi Mungu ambao ni huruma radhi na Pepo, mpaka mutoe katika vile mvipendavyo, kwa maana: Mali kwa ujumla au vingine ([37]). Na Mwenyezi Mungu Akasema katika sifa za waja wema:

{Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa} Al-Insaan: 8. Ndani ya Aya Tukufu neno “Kukipenda kwake” makusudio yake ni kupenda chakula pamoja na ladha yake na kukihitaji, au kwa kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu ([38]).

Kutoa mali na kuipata mwanadamu ni ukamilifu wa nguvu ya nafsi yake kwa kufanya huruma kwa waja wa Mwenyezi Mungu, hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawajibisha zaka ili kufikia roho ya ukamilifu huu nao ni uadilifu wa kuwa kwake mwema kwa viumbe na akifanya juhudi za kufikisha kheiri kwao na kuondoa matatizo yao ([39]).

Sharia Takatifu katika utekelezaji wa zaka na mfano wake imewajibisha kuepukana na kujiona mtoaji na kuleta maudhi kwa zaka yake, kufanya hivyo huaribu na kubatilisha malipo yake, Mola Mtukufu Amesema:

{Wanao toa mali zao kwa Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishii simulizi wala udhia kwa walichotoa, wana malipo yao kwa Mola wao Mlezi, wala hawatakuwa na hofu juu yao wala kuhuzunika} Al-Baqarah: 262.

Na akasema tena: {Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadakainayo fuatiliwa na maudhi} Al-Baqarah: 263.

HIJA:

Hija ni nguzo katika nguzo za Uislamu, ni wajibu kwa mwenye kuweza kuitekeleza, kwani imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary pamoja na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Hija njema malipo yake ni Pepo” na imepokewa Hadithi nyingine kutoka kwa Jabiri Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Hija njema malipo yake ni Pepo”, wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nini wema wa Hija njema? Akasema: “Kulisha chakula na kutoa salamu”.

Hija ina nguzo wajibu na yanayopendeza kufanywa, na katika yanayopendeza kufanywa ni pamoja na: Kugusa jiwe jeusi, kwa mwenye kuhiji kwa kuweka mkono yake na kulibusu, kwani imepokewa na Imamu An-Nasaai kutoka kwa Ibn Abbas R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Jiwe jeusi ni katika mawe ya Peponi”.

Pamoja na hayo ikiwa kufanya hivyo kutapelekea kuleta msongamano kwa wengine pamoja na kuleta maudhi basi haihitajiki kufanya hilo, “Kwa sababu kuligusa ni Sunna, na kuondoa kero na maudhi ni jambo la lazima, hivyo kutekeleza la wajibu ni lazima” ([40]), hii ni katika hukumu ambayo inaonesha pia maana ya wema.

Mashirikiano:

Ama mashirikiano ni katika wema uliowazi katika hukumu zinazotokana na mlango huu, katika mifano ya mashirikiano:

 Kutakiwa umakini katika kazi anayoifanya mwanadamu iwe ya kwake mwenyewe au ya mtu mwingine, imepokewa na Imamu Twabrany katika kitabu chake kutoka kwa Bibi Aisha R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Anapenda mmoja wenu anapofanya kazi kuifanya kwa umakini”.

Wajibu wa kusema ukweli kati ya wanaokubaliana na uharamu wa kufanya ulaghai, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Hakim Ibn Hizam R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Wawili wenye kuuziana wana hiyari kabla ya kuachana – au amesema hata baada ya kuachana – ikiwa watakuwa wakweli na wawazi basi watabarikiwa kwenye biashara yao, na ikiwa watafichana na kuongopeana itaondolewa baraka kwenye biashara yao”.

Na imepokewa na Imamu Muslimu na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kufanya udanganyifu si katika sisi”.

Uharamu wa mtu kuuza alichouziwa ndugu yake au kununua alichonunua, kwa mnunuzi kutoa bei ya chini zaidi ya ile aliyotaka kununua mwanzo, au kumzidishia bei zaidi ya ile aliyotaka kununua baada ya kuthibiti bei, hii ni kutokana na kuwepo kero, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Imamu Muslimu kutoka kwa Ibn Omar R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Mmoja wenu asiuze alichouziwa ndugu yake”.

Kutakiwa usamehevu katika mashirikiano na mwingine ya kuuza kununua au jambo lingine, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Mwenyezi Mungu humrehemu mtu mwenye kusamehe pindi anapouza anaponunua na anapodai deni”, katika Hadithi hii umehimizwa wema kwa waja kwa kuhimizwa usamehevu, ushirikiano mzuri, kutumika tabia nzuri na kuacha magonvi katika kuuza, hilo ni kwa sababu ya uwepo wa baraka ndani yake, na kauli yake S.A.W “Na anapodai deni” amehimiza kuacha kuwabana watu wakati wa kutaka haki na kuwa msamehevu kwao ([41]).

Na imepokewa na Baihaqy kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:  “Mwenye kumuondolea mwenye kujuta tatizo la bidhaa aliyonunua. Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsamehe makosa yake siku ya Kiyama” ([42]).

Kupendeza kutoa msamaha kwa mdaiwa aliyekwama ambaye muda wa kutakiwa kulipa deni lake umekaribia lakini hana uwezo wa kulipa, au kumsubiria mpaka pale atakapoweza kulipa, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: 

{Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkilifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua} Al-Baqarah: 280. Kwa maana ikiwa mdaiwa ana hali ngumu basi msubirieni mpaka atakapoweza kulipa, na mtoe sadaka, kwa maana kuacha asili ya mali ambayo mumewapa kama deni kwa kuliachia lote au sehemu yake basi mwisho wa hilo ni bora kwenu ikiwa mnajua kuwa ni bora basi fanyieni kazi ([43]).

Uharamu wa ukiritimba wa bidhaa muhimu ambayo ni chakula cha watu, kwa mtu kununua wakati wa bei ya juu, ili kukiuza kwa bei ya juu zaidi alivyonunulia wakati wa kuhitajika sana ([44]), na hilo ni kutokana na uwepo wa kero na maudhi kwa watu, imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Miimar Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Hafanyi ukiritimba isipokuwa ni mwenye makosa” mwenye makosa: Ni mtu muasi na mwenye dhambi, na Hadithi hii ipo wazi katika kuelezea uharamu wa ukiritimba. Wanachuoni wamesema: Hekima katika uharamu wa ukuritimba ni kuondoa madhara kwa watu ([45]).

Ndoa Talak ana Masuala ya Kanuni za Ndoa.

Uhusiano wa ndoa ni uhusiano mtakatifu, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameusifu kuma ni ahadi madhubuti, akasema kwenye kauli yake:

{Na mtachukuaje na hali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti} An-Nisaai: 21. Kwa maana ahadi nzito ([46]), hivyo Sharia Takatifu imeweka wazi uhusiano huu kwa jumla ya hukumu ambazo zinatumika kumuumba mwanadamu ikiwa kulinda huu uhusiano na kutukuza nafasi yake, miongoni mwa hizo hukumu ni:

Kumtaka ruhusa mwanamke kabla ya kumuoa, kwa sababu utashi wake na matakwa yake yanaheshimika, na ikiwa mwanamke mkubwa mwenye akili asiye na bikra ataolewa bila ya ruhusa yake basi ndoa yake itapitishwa na yeye mwenyewe, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary pamoja na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Haolewi mwanamke asie bikra mpaka kwa amri yake, wala haolewi mwanamka bikra isipokuwa atakwe ruhusa”.

Kutakiwa kufanya wema kwa mke, kwa kumfanyia upole na kumuondolea matatizo yake na kumsaidia kadiri uwezavyo, na mume kulipwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa yale anayomfanyia mke wake kama kuhudumia chakula chake na mfano wake, imepokewa na Imamu Bukhary na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Wausieni wake zenu mambo mazuri”.

Na imepokewa na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Bibi Aisha R.A Mtume S.A.W amesema: “Kwa hakika katika Waumini wenye imani kamili ni wale wenye tabia nzuri zaidi na wapole kwa familia zao”.

Na Mtume S.A.W amesema pia: “Mbora wenu ni yule aliyembora kwa familia yake, na mimi ni mbora wenu kwa familia yangu”.

Imepokewa na Imamu Bukhary kuwa Bibi Aisha R.A aliulizwa: Ni mambo gani Mtume S.A.W alikuwa akifanya nyumbani kwake? Akasema: “Alikuwa akifanya kazi za kuhudumia familia yake, pindi unapoingia wakati wa Swala alikuwa akitoka kwenda kuswali”.

Na imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Muumini wa kiume hamkasirikii Muumini wa kike, ikiwa atamchukiza kwa tabia moja basi humridhia kwa tabia nyingine”.

Imepokewa na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Masoud Al-Badri R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Kwa hakika Muislamu anapofanya matumizi kwa familia yake naye akafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi kwake inakuwa ni sadaka”.

Na imepokewa pia na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Dharri Al-Ghaffary kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Katika tupu ya mmoja wenu ni sadaka. Wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi mmoja wetu akafikwa na matamanio yake atakuwa na malipo? Akasema: Hivi mnaonaje lau tupu yake ataiweka kwenye haramu hatokuwa na dhambi? Vile vile ikiwa ataiweka katika halali anakuwa na malipo”.

Mwanamke kutakiwa kuheshimu nafasi ya mume wake na wajibu wa kumtii katika mambo yasiyo ya maasi, imepokewa Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Lau ningeamrisha mtu yeyote kumsujudia mtu basi ningeamrisha mwanamke kumsujudia mume wake”.

Na imepokewa pia Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Ummu Salama R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Mwanamke yeyote akifariki na mume wake akiwa radhi naye ataingia Peponi”.

Wajibu wa uadilifu kati ya wake, imepokewa Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Ikiwa mwanamme ana wake wawili wala hakufanya uadilifu kati yao basi siku ya Kiyama atakuja bega lake moja likiwa limeinama”. Ikasemwa ataonekana na watu ili hii iwe ni ongezeko kwake ka adhabu ([47]).

Wajibu wa kumfanyia wema mke aliyeachwa kwa mwanamme kutomuacha katika eda yake mpaka inapokaribia kuisha kisha anamrejea tena, si kwa kitu chochote isipokuwa ni kutaka kumletea madhara ya kurefuka kwa eda yake, bali amrejee si kwa kutaka kumletea madhara kwa kumrejea, au kumuacha tu mpaka kumalizika eda yake pasi ya kumfanyia madhara. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Talaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri} Al-Baqarah: 229.

Na akasema tena:

{Na mtakapo wapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waacheni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye fanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake} Al-Baqarah: 23. Mwenyezi Mungu Akasema tena: {Wala msisahau fadhila kati yenu} Al-Baqarah: 237.

Adhabu:

Uislamu umeweka adhabu za kukemea kufanya sababu zake, si katika makusudi yake kujitosheleza matamanio ya kuadhibu watu, bali yenyewe ni katika hatua ya kuondoa uharibifu kwa jamii yote hasa mtu anapata tabu kufanya uhalifu kwa mwengine pindi anapoona adhabu kwa mtu aliyeadhibiwa, pamoja na hayo kufanyia kazi hii adhabu kuna masharti yanayobana sana wigo wake, kwa maelezo zaidi utafahamu kwenye marejeo yake maalum.

Imewekwa Sharia ya adhabu hii kwa hekima iliyotajwa ikiwa ni aina katika aina za wema, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari} Al-Mulku: 14. Na kutekelezwa kwa sura ya Kisharia pia ni aina katika aina ya wema, na miongoni mwa sura za wema katika mlango wa adhabu za Kisharia ni kama zifuatazo:

Kuondolewa adhabu kwa mtuhumiwa ikiwa kutapatikana shaka au akiwa na sehemu halali ya kutokea, imepokewa Hadithi na Baihqy kutoka kwa Bibi Aisha R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Ondoeni adhabu kwa Waislamu kadiri mnavyoweza, ikiwa kwa Muislamu mtakuta sehemu ya kutokea basi muachieni huru, kwani kiongozi kukosea kutoa msamaha ni bora kwake kuliko kukosea kutoa adhabu”.

Mwanadamu anahitajika kustiri nafsi yake iwapo atakiuka sehemu ya wajibu, na atubu kati yake na Mwenyezi Mungu, wala asikili yeye mwenyewe ili itekelezwa adhabu juu yake, kwani imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema: Nimemsikia Mtume S.A.W anasema:

“Umma wangu ni wenye kusamehewa isipokuwa wenye kujidhihirisha, miongoni mwa kujidhihirisha mja amefanya jambo usiku kisha anaamka asubuhi akiwa Mola amemsitiri anasema: Ewe fulani nimefanya baya hili na hili, akiwa amelala Mola amemstiri, anaamka asubuhi anaweka wazi sitara ya Mwenyezi Mungu kwake”.

Imepokewa na Maliki kutoka kwa Zaidi Ibn Aslama R.A kuwa kuna mtu mmoja katika enzi za Mtume S.A.W alikiri yeye mwenyewe kuwa amefanya kitendo cha uzinifu, ndipo Mtume S.A.W alimuita kwa mjeledi na akachapwa viboko, kisha akasema: “Enyi watu ni wakati wenu kufahamu adhabu za Mwenyezi Mungu, mwenye kufanya huu uchafu na akasitirika kwa sitara ya Mwenyezi Mungu, kisha yeye akatuonesha ukurasa wake basi tutatekeleza kwake hukumu za Kitabu cha Mwenyezi Mungu”.

Usawa na kuto bagua katika kutekeleza adhabu, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Bibi Aisha R.A kuwa Makuraishi walikuwa na wasi wasi juu ya suala la mwanamke wa Makhzumiya ambaye aliiba na wakasema: Nani atamuambia Mtume wa Mwenyezi Mungu? Wakasema: Mwenye uthubutu kwake ni Usama Ibn Zaidi, hivyo Usama akamueleza Mtume S.A.W na Mtume akasema: “Hivi mnamuombea msamaha katika adhabu ya Mwenyezi Mungu?” kisha akasimama na kutoa hutuba akasema:

“Kwa hakika waliangamia watu kabla yenu kwa sababu walikuwa pindi anapoiba miongoni mwao mtu mwenye heshima wanamuacha, na anapoiba mtu mnyonge wanatekeleza kwake adhabu, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu lau Fatuma binti Muhammad angeiba basi ningemkata mkono wake”.

Adhabu ikiwa ni kifo basi yaepukwe mateso bali atauliwa kwa kutumia chombo chenye makali kitakacho muuwa haraka sana pasi ya maumivu makali sana, wala haifai kuuchezea mwili kabla na hata baada ya adhabu, kwani imetangulia kutajwa Hadithi ya Imamu Muslimu kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Hakika Mwenyezi Mungu ameandika wema juu ya kila kitu, ikiwa mtaua basi uweni kwa uzuri”, na imepokewa Hadithi pia na Imamu Bukhary kutoka kwa Abdillah Ibn Yazid R.A kuwa Mtume S.A.W amekataza kuuadhibu mwili wa mtu aliyeuwawa kwa kukata viungo vyake na kuchafua umbo lake kabla au hata baada ya kuuwawa ([48]).

Kuhitajika ndugu wa marehemu kutoa msamaha kwa mhalifu wa kosa la jinai katika ulipizaji kisasi, kwa sababu ni haki yao inaweza kuondoka kwa kusamehe kwao, Mola Mtukufu Anasema:

{Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uwawa - muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe kwa ihsani} Al-Baqarah: 178. Kwa maana mwenye kusamehewa na ndugu wa marehemu kutokana na uhalifu wake, na ikatajwa kwa tamko la ndugu uliothibiti kati yao kwa upande wa ubinadamu na Uislamu:

{Basi na alipe kwa wema} kwa maana afuatilizie wema, na kusudio lake: Ni wasia kwa msamehevu kupewa fidia kwa wema bila ya kutumia nguvu, na mwenye kusamehewa anapaswa kutekeleza fidia hiyo kwa wema: Asicheleweshe wala kupunguza ([49]).

Na Mwenyezi Mungu Amesema:

{Na humo tuliwaandikia ya kwamba roho kwa roho, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na kwa majeraha kuna ulipizaji kisasi. Lakini atakaye samehe basi itakuwa ni kafara kwake} Al-Maidah: 45. Kwa maana mwenye kusamehe na akaacha kulipiza basi huo ni msamaha wake kwa Mwenyezi Mungu na ni thawabu kubwa ([50]).

Imepokewa Hadithi na Abu Daud kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A amesema:

“Sijamuona Mtume S.A.W ikipelekwa kwake kesi yenye kuhitajika ulipazaji kisasi, isipokuwa aliamrisha kusamehe”.

Jihadi na Mahusiano ya Kimataifa

Vita na mapigano ni tukio la kijamii la kibinadamu amekuwa nalo tokea enzi, ni kwa sababu ya mvutano kati ya mwanadamu ambaye lazima azae aina ya mgongano, Mwanachuoni Ibn Khaldun anasema katika utangulizi wa historia yake: “Fahamu kuwa vita na aina mbalimbali za mauaji bado vimeendelea kutokea katika uongozi tokea Mwenyezi Mungu alipoumba, na asili yake na utashi wa watu wao kwa wao kulipiza kisasi, na kufanya ugonvi kila mmoja kwa mgonvi wake, pindi wanapohimizana kwenye hilo na makundi mawili yakakubaliana, kundi moja litataka kulipiza kisasi na kundi lingine litajilinda, ndipo kunapokuwa na vita, ni jambo la kawaida kwa mwanadamu haliwezi kuepukwa na Umma wala kizazi, na sababu ya ulipizaji huu mara nyingi ima wivu na ushindani, ima uadui, ima hasira za kutaka kumiliki” ([51]).

Na katika uwanja huu ambao utakuwa na vita mauaji umwagaji damu na uharibifu Uislamu umejikunjua kwa sura nzuri zaidi ili kuwaonesha wanadamu roho ya wema katika hukumu zinazohusu mlango huu, miongoni mwa wema huo:

Kusimamia uhuru wa imani na uharamu wa kutenza nguvu mtu kuingia katika dini. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Hakuna kulazimisha katika dini} Al-Baqarah: 256.

Uharamu wa kuuwa wanawake na watoto wadogo wasiopigana vita, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Abdillah Ibn Omar R.A kuwa, kuna mwanamke mmoja alikutwa ameuwawa katika moja ya vita vya Mtume S.A.W basi Mtume alikasirika kuuwa wanawake na watoto wadogo, na katika mapokezi mengine: Mtume S.A.W alikataza kuuwa wanawake na watoto wadogo.

Uharamu wa kutumia moto vitani kumuunguza adui, madamu anaweza kumfanya jambo lingine, imepokewa Hadithi na Abu Daud kuwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna anayeadhibu kwa moto isipokuwa Mola wa moto”. Na katika Aya zinazokusanya mlango huu ni pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui} Al-Baqarah: 190. Kwa maana: Piganeni ili kuinua neno lake na kuipa nguvu dini yake, wala msifanye uadui kwa kuanza vita au kumshambulia mtu wa mwenye makubaliano naye, au kumstukiza tu bila ya kuwa na taarifa, au kuuchezea mwili wake, au kumuua mliokatazwa kumuua ([52]).

Katika Suala la Mahusiano ya Kimataifa

Wajibu wa kutekeleza makubaliano mikataba na ahadi za Kimataifa ambazo zimeridhiwa na nchi za Kiislamu na kujiunga kwenye makubaliano hayo na kuyapitisha kwa utashi wao na kwa hiyari yao na uharamu wa kuyavunja, kwa sababu yenyewe baada ya kufikiwa yanakuwa na makubaliano na mikataba iliyosainiwa, hivyo ni lazima kutekelezwa yale yaliyofikiwa makubaliano. Mwenyezi Mungu Anasema: {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi} Al-Maidah: 1. Na utimizaji: Ni kulinda makubaliano na kuyatekeleza ([53]), na mkataba ni uwingi wa mikataba, mkataba hutumika kila kilichowajibu kati ya pande mbili kufanya kitu fulani, na Aya kwa ujumla inawajibisha na kulazimisha kutekeleza na kutimiza makubaliano yote ([54]), imepokewa Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Amr Ibn Auf Al-Mazni R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Waislamu wapo kwenye sharti zao, isipokuwa sharti la kuharamisha halali au kuhalalisha haramu”. Na imepokewa pia Hadithi na Abu Daud kutoka kwa Amr Ibn Abasa R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Mwenye kuwa na makubaliano kati yake na watu wengine basi asikiuke makubaliano mpaka muda wake uishe au kuwajulisha”. Kauli yake: “Asikiuke makubaliano” hii ina maana ya kulinda makubaliano na kutoyabadilisha au kuyavunja, na kauli yake: “Kuwajulisha” kwa maana kuwatupia makubaliano, kwa kuwapa taarifa kuwa yeye amevunja makubaliano kutokana na hali ya wasi wasi wa kufanyika hiyana kutoka kwao, ili mgonvi wake awe sawa sawa na yeye katika kuvunja makubaliano hayo ili kusiwe na udhuru wowote ([55]).

Na imepokewa Hadithi na Abu Daud kutoka kwa Abi Rafii R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Hakika yangu mimi sivunji makubaliano”, kwa maana si vunji makubaliano wala kuyaharibu, Imamu Al-Khattabi amesema katika sherehe yake: “Wapo Wanachuoni wanasema: Makubalianao na kafiri yanazingatiwa kama makubaliano na Muislamu, na kafiri anapoingia makubaliano na wewe makubaliano ya amani basi umewajibikiwa kumpa amani, wala usishambulie damu yake wala mali yake wala manufaa yake” ([56]).

Uharamu wa kuwasaliti wasiokuwa Waislamu wakati wanapokuwa wameingia kwa amani katika nchi za Kiislamu, vile vile hali kama hiyo kwa upande wa Muislamu anapoingia nchi si ya Waislamu kwa kuwa na viza ya kuingia na mfano wake kwani anakuwa ni wa kulindwa, wala haifai kwake kufanyiwa ukiukwaji wowote au kusalitiwa, damu zao mali zao na heshima zao zinakuwa ni haramu, ikiwa atafanyiwa uadui juu ya kimoja wapo inakuwa ni hiyana na usaliti kwao, kwa sababu viza ya kuingia wasio Waislamu ndani ya nchi za Waislamu ndio makubaliano ya amani, vile vile kwa upande wa Muislamu kuingia nchi si ya Waislamu, kwa sababu wao hawakumpa viza isipokuwa kwa sharti la kuacha kuwasaliti na nafsi zao kuwa na amani, na hili ikiwa halijatajwa kwenye mkataba lakini linafahamika katika maana, na makubaliano ya amani yanapelekea pande zote mbili za makubaliano kuaminiana na kila mmoja anamuhakikishia mwenzake usalama, wakati huo haiwi kwa Muislamu hiyana wala usaliti, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Abdillah Ibn Amr R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: 

“Mambo manne mtu akiwa nayo anakuwa ni mnafiki moja kwa moja, na mwenye kuwa na jambo moja kati ya hayo anakuwa na sehemu ya unafiki mpaka aache. Anapoaminiwa hufanya hiyana, anapozungumza huwongopa, anapo ahidi hatekelezi ahadi, na anapogombana hufanya uovu”.

Na imepokewa Hadithi pia na Imamu Muslimu kutoka kwa Ibn Omar R.A Mtume S.A.W amesema:

“Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama atakapo wakusanya watu wa mwanzo na wa mwisho, basi msaliti atainua bendera, patasemwa: Huyu alimsaliti fulani Ibn fulani”.

Kiapo:

Katika mlango wa kiapo na yamini inatakiwa mtu avunje kiapo chake na kukipinga ikiwa kimefungamana na jambo lenye uadui au kero au amepata kilichobora zaidi tofauti na kile alichokiapia, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Abi Musa Al-Ashary R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Hakika yangu mimi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu si api kiapo, kisha nikaona kilichobora zaidi ya kiapo isipokuwa navunja kiapo changu na ninafuata kile kilichobora zaidi”.

Kulisha na Kunywesha:

Chakula na kinywaji ni katika mahitaji ya msingi ya mwanadamu ambayo Uislamu umeweka katika mizani ya wema, katika mizani hiyo:

Kuzuia matumizi mabaya. Mwenyezi Mungu Amesema: 

{Na kuleni, na kunyweni wala msifanye ubadhilifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya ubadhilifu} Al-Aaraf: 31.

Kutukuza neema kwa kuacha kutaja aibu ya chakula, kama vile kukiaibisha kunaweza kuvunja heshima ya mwenye chakula au mpishi, na imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema:

“Mtume S.A.W hajawahi kabisa kukitia kasoro chakula, ikiwa amekipenda anakila, na kama hakipendi hukiacha”.

Kuwinda na Kuchinga:

Tabia za wema huonekana katika mlango huu katika vingi, miongoni mwa hivyo: Kutakiwa kuchinja vizuri wanyama kunakopelekea kumpunguzia maumivu mnyama aliyechinjwa kadiri inavyowezekana, mtu anatakiwa kunoa kisu chake kabla ya kuchinja, na amzuie mnyama kwa kutumia chombo kisichokata, kuepusha kunoa kisu mbele ya mnyama, au kuchinja mnyama mmoja mbele ya mwingine, na kutomkata sehemu ya kiungo chake kabla kuondoa roho yake, yote hayo ni katika kumuadhibu mnyama, yanakusanywa haya yote na mengine ni katika mambo ya wema, katika Hadithi iliyopokewa na Imamu Muslimu kutoka kwa Shaddad Ibn Ausi R.A amesema: Mambo mawili yamehifadhiwa na Mtume S.A.W akasema:

“Hakika Mwenyezi Mungu ameandika wema kwenye kila kitu, ikiwa mutauwa basi uweni vizuri, ikiwa mtachinja chinjeni vizuri, na mmoja wenu anoe kisu chake na amuondolee maumivu mnyama wake”.

Mashirikiano Mtumwa na Mhudumu

Sharia ya Kiislamu imekuja kwa walimwengu wote, na mfumo wa utumwa umekuwa upo wenye kusimama maeneo mbalimbali, Sharia ya Kiislamu ikawema mfumo wa hukumu zinazotengeneza uhusiano kati ya bwana na mtumwa wake msingi wake ni kutengeneza wema pia, miongoni mwa mfumo huo:

Kuhimiza kumuacha huru mtumwa, mpaka kuacha huru mtumwa kumekuwa ni ibada ambayo mja anajiweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusababisha kufutiwa madhambi, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema:

“Mwenye kumuacha huru mtumwa, Mwenyezi Mungu atakiacha huru kila kiungo katika viungo vyake na adhabu ya moto”. Na kuachwa huru mtumwa imefanywa ni kafara ya kumpiga mtumwa, imepokewa Hadithi na Ahmad kutoka kwa Ibn Omar R.A Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kumpiga mtoto wake kafara yake ni kumuacha huru mtumwa”.

Kuhimiza kuchunga ubinadamu wa mtumwa katika kushirikiana na kutomfanyisha kazi asiyoiweza, imepokewa pia Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Abi Dharri Al-Ghaffary R.A Mtume S.A.W amesema:

“Wao ni ndugu zenu, Mwenyezi Mungu amewafanya kuwa chini ya usimamizi wenu, hivyo walisheni kile mnachokula, wavisheni kile mnachovaa, wala msiwafanyishe kazi zinazowashinda, ikiwa mtawafanyisha kazi basi wasaidieni”.

Ama mhudumu asiye mtumwa Mtume S.A.W ametufanyia mfano bora katika kuwafanyia wema, imepokewa Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A amesema:

“Nimefanya kazi kwa Mtume S.A.W miaka kumi, hajawahi kuniambia hata neno: Aah, na wala hajawahi kuniambia kitu nilichokifanya: Kwanini umefanya? Wala kuacha kitu: Kwanini umeacha? Na Mtume S.A.W alikuwa ni mbora zaidi wa tabia”.

Imepokewa Hadithi na Ahmad katika Musnadi yake kutoka kwa Bibi Aisha R.A amesema:

“Sijawahi kabisa kumuona Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W akimpiga mtumishi, wala mwanamke, wala mkono wake kupiga chochote, isipokuwa katika jihadi kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu, wala hajafanyiwa jambo akataka kulipiza kisasa kwa mfanyaji, isipokuwa ikiwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikiwa ni jambo la Mwenyezi Mungu hutekeleza kisasi”.

Kufnayia Wema Nafsi:

Uislamu umeweka hukumu nyingi ambazo zinaonesha maana ya wema kuhusu ushirika wa mwanadamu na nafsi yake na mwili wake, miongoni mwa hukumu hizo:

Uharamu wa mwanadamu kujiuwa mwenyewe. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anaesema: {Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mwingi wa huruma} An-Nisaai: 29. Na Akasema tena:

{Aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote} Al-Maidah: 32.

Imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Thabit Ibn Dhahak R.A Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kujiua mwenyewe na kitu chochote basi ataadhibiwa nacho ndani ya moto wa Jahannam”.

Ulazima wa kulinda akili, na uharamu wa kuipa kianachoiondoa, kama vile pombe na mfano wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa} Al-Maidah: 90.

Na imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Bibi Aisha R.A Mtume S.A.W amesema:  كُ “Kila kinywaji kinacholewesha ni haramu”.

Kutafuta dawa kutokana na maradhi ili kulinda afya, imepokewa Hadithi na Abu Daud kutoka kwa Abi Dardai R.A Mtume S.A.W amesema:

“Hakika Mwenyezi Mungu ameteremsha ugonjwa na dawa, na akafanya kila ugonjwa una dawa, hivyo tafuteni dawa, na wala msitafute dawa kwa vitu vilivyoharamu”.

Kutafuta kujipamba maeneo ya nje ya mwili na kuonesha neema ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi, imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Abdillah Ibn Masoud R.A Mtume S.A.W aliulizwa: Hakika mtu anapenda nguo yake kuwa nzuri na viatu vyake kuwa vizuri, akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu Mzuri na Anapenda uzuri”.

Na imepokewa Hadithi na Imamu Tirimidhy kutoka kwa Amr Ibn Shuaibu kutoka kwa baba yake kuotoka kwa babu yake amesema: Mtume S.A.W amesema

“Hakika Mwenyezi Mungu Anapenda kuona athari ya neema yake kwa mja wake”.

Hukumu hizi zote zinakusanywa na kauli ya Mtume S.A.W iliyopokewa na Baihaqy – Asili yake ipo kwenye kitabu cha Sahihi ya Imamu Bukhary – kutoka kwa Juhaifah R.A Mtume S.A.W alisema kumuambia Abi Dardai R.A: “Hakika mwili wako una haki kwako”, na tamko la Imamu Bukhary ni: “Nafsi yako” badala ya “Mwili wako” nayo ni katika jumla ya maneno ya Mtume S.A.W

Kufanya Wema kwa Watu Wote kwa Aina zao Mbalimbali:

Hukumu za Sharia zimekuja zikiamrisha tabia ya wema katika kushirikiana na mtu mwingine, na linaonekana hilo kama ifuatavyo:

Katika haki za wazazi wawili. Mola Mtukufu Anasema: {Na wafanyieni wema wazazi wawili} An-Nisaai: 36. Na imepokewa na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema: Kuna mtu alikuja kwa Mtume S.A.W na kumuuliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni mtu gani ana haki zaidi ya kumfanyia wema? Mtume akasema: Mama yako, akauliza: Kisha nani? Mtume akasema: Mama yako, akauliza: Kisha nani? Mtume akasema: Mama yako, akauliza kisha nani? Mtume akasema: Baba yako”.

Na katika haki za watoto, imepokewa Hadithi na Abu Daud kutoka kwa Nuuman Ibn Bashiir R.A Mtume S.A.W amesema kumuambia baba yake Nuuman:  “Hakika ni haki yao kwako kufanya uadilifu kati yao, kama vile wao kwao una haki ya kukufanyiwa wema”.

Katika haki ya watu wa karibu, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema: Nimemsikia Mtume S.A.W anasema:

“Mwenye kutaka afunguliwe riziki yake, na kuzidishiwa baraka katika umri wake, basi na aunge ndugu zake”.

Na katika haki ya jirani, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary na Muslimu kutoka kwa Ibn Omar R.A amesema: Mtume S.A.W amesema: 

“Malaika Jibril hakuacha kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhani atamrithisha”. Kwa maana atakuja na amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya jirani kumrithi jirani yake ([57]).

Imepokewa pia Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Abi Sharih R.A Mtume S.A.W amesema:

“Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hana imani, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hana imani, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hana imani. Akaulizwa ni nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ambaye jirani yake hana amani kwa mdomo wake” ([58]).

Katika haki ya mgeni, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi amkirimu mgeni”. Na kutoka kwa Abdillah Ibn Amr R.A Mtume S.A.W amesema: “Kwa hakika mgeni wako kwako ana haki”.

Katika haki za mjane na masikini, imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema:

“Mwenye kwenda mbio kusaidia mjane na masikini, ni kama mpigania jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kusimama usiku na kufunga mchana”.

Katika haki za Waislamu na watu wote, imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema:

“Mwenye kumuondolea Muumini tatizo katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamuondolea matatizo ya siku ya Kiyama, na mwenye kumfanyia wepesi mwenye tatizo, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na mwenye kumstiri Muislamu Mwenyezi Mungu atamstiri duniani na Akhera, Mwenyezi Mungu humsaidia mja ikiwa mja anamsaidia ndugu yake”.

Na imepokewa pia Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Masoud Al-Answary R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kuonesha jambo la kheiri basi ana malipo mfano wa malipo ya mtendaji wake”.

Imepokewa Hadithi na Imamu Ahmad katika Musnadi yake kutoka kwa Aqaba Ibn Aamir R.A amesema: Nilikutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W akaniambia:

“Ewe Aqaba Ibn Aamir, muunge undugu aliyekukata undugu, mpe aliyekunyima na msamehe mtu aliyekudhulumu”.

Kufanya Wema kwa Wanyama:

Katika Sharia ya Kiislamu wema hausimami kwa viumbe wenye akili tu bali unavuka na kwenda mpaka kwa wanyama pia, imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Jarii R.A Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kunyimwa huruma amenyimwa kheiri”.

Na imepokewa pia Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema:

“Kuna mtu alikuwa njiani akafikwa na kiu kikali na akakuta kisima, akaingia kisimani na kuchota maji na kunywa kisha akatoka, mara akamuona mbwa anabweka akiwa ameshikwa na kiu, yule mtu akasema: Kwa hakika mbwa huyu amefikwa na kiu kama kilichonifika mimi, hivyo akaingia tena kisimani na akaja na maji kwenye kiatu chake na kumnywesha mbwa basi akamshukuru Mwenyezi Mungu na akasamehewa dhambi zake. Maswahaba wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi sisi katika wanyama tuna malipo? Mtume S.A.W akasema: Katika kila kiumbe chenye maini mabichi kuna malipo”.

Imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema:

“Kuna mwanamke muovu alimuona mbwa siku ya joto kali akizunguka pembezoni mwa kisima, akiwa ametoa ulimu wake kutokana na kiu, akavua kiatu chake na kumpa maji akasemehewa dhambi zake”.

Imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Ibn Omar R.A Mtume S.A.W amesema: “Mwanamke ameingia motoni kwa sababu ya paka alimfunga bila ya kumpa chakula, na wala hakumuacha ale vijidudu ardhini” ([59]).

Imepokewa Hadithi na Imamu Ahmad katika Musnadi yake kutoka kwa Muadhi Ibn Anas Al-Jahny R.A Mtume S.A.W siku moja alipita kwa watu wakiwa wamesimama na wanyama wao na mizigo yao, akawaambia:

“Wapandeni kwa usalama na waacheni kwa usalama, wala msiwanye viti vya kukalia kwa ajili ya mazungumzo yenu barabarani na masokoni, kwani huenda anayepandwa akawa ni mbora zaidi ya mpandaji, na mtajeni sana Mwenyezi Mungu Mtukufu”.

Imepokewa na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Abdillah Ibn Amr R.A Mtume S.A.W amesema: “Watu wenye huruma Mwenyezi Mungu huwahurumia, wahurumieni waliopo ardhini watawahurumia waliopo mbinguni”.

Waislamu kwa muda mrefu wamefahamu hii huruma kwa kina, na wakatekeleza vizuri adabu hii ya Mtume, hivyo wakatumia ofisi za Waqfu kulelea wanyama, pamoja na rai za Jamhuri ya Wanasharia wanaona najisi aliyonayo mbwa ([60]), isipokuwa hilo halikuwa kizuizi katika kuwafanyia wema mbwa na kuwafanyia huruma kama viumbe hai katika viumbe vya Mwenyezi Mungu, wakatumia Waqfu kuhudumia matembezi ya mbwa na vituo vya mbwa waliokosa mafunzo, nayo ni Waqfu faida yake hutumika kuhudumia mbwa ambao hawana wenyewe wanaowasimamia, ili kumuokoa na adhabu ya njaa ili wanusurike na kifo, na kulikuwa na Waqfu ya kuhudumia ngamia wasioweza kufanya kazi, na mji wa Al-Marji Al-Akhdhar huko Damascus kulikuwa na Waqfu ya kuhudumia wanyama wenye umri mkubwa wapate chakula mpaka vifo vyao pasi ya kulazimika mwenye mnyama kumuua ili kuepukana na kumuhudumia, na kulikuwa na Waqfu kwa ajili ya kuuguza paka mbwa na wanyama wengine wanaoumwa na kuwalea wanapo zeeka, na Waqfu ya Al-Ghulal ambayo uhudumia chakula cha ndege wa angani ([61]).

Kufanya Wema kwa Visivyo na Uhai:

Wema katika hukumu za Kiislamu umevuka mipaka, mpaka umefika kwenye vitu visivyo hai na usikivu ambavyo havina roho wala akili, Muislamu anaona kuwa vitu visivyo na uhai hata kama vimetulia bali vipo kwenye ibada ya ndani ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kuleta tasbihi na kumshuhudia Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Anasema:

{Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye msamaha} Al-Israa: 44. Baadhi ya waja wema wanakunjuliwa hali hii isiyofahamika hivyo wanaona au wanasikia kwa hasia za wazi kwa sura ya karama na miujiza, na imekuja katika vitabu vya Sunna Takatifu tasbihi ya jiwe mbele ya Mtume S.A.W, na imepokewa Hadithi na Imamu Bukhary kutoka kwa Ibn Masoud R.A amesema: “Tulikuwa tunasikia tasbihi ya chakula kikiwa kinaliwa”.

Sheikh Muhyiddiin Ibn Al-Araby Al-Haatimiy Al-Andulus amesema: “Kwetu jiwe na vitu visivyo na uhai viko tofauti na watu wanavyoviona, kama Mwenyezi Mungu Allivyosema: 

{Kwani kuna mawe yanayo tumbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumuogopa Mwenyezi Mungu} Al-Baqarah: 74. Ameyaelezea kwa sifa ya hofu na zenginezo, na Mwenyezi Mungu Akasema: {Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur`ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu} Al-Hashru: 21. Na Mwenyezi Mungu Akasema:

{Kwa hakika Sisi tulifikisha amana kwa mbingu na ardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa} Al-Ahzab: 72. Na Mwenyezi Mungu Akasema kuiambia mbingu na ardhi:  {Njooni, kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni watiifu} Fussilat: 11. Mola Akasema tena: {Enyi milima! Karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia} Sabai: 10. Kwa maana rudieni kutakasa na nendeni nazo, na Mola Akasema: {Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake} Swaad: 36. Na Mtume S.A.W amesema:

“Hakika Mimi ninafahamu jiwe lilikuwa linanisalimia” ([62]). Na akasema katika Uhudi: “Huu ni mlima unatupenda na tunaupenda” ([63]). Na Nabii Musa A.S amesema: “Nguo yangu jiwe, nguo yangu jiwe” ([64]), akiita na kijiwe kikimtaja Mwenyezi Mungu katika kiganja cha Mtume S.A.W na yanayofanana na hayo, vitu visivyo hai kwetu sisi ni alama ya Mwenyezi Mungu yenye kutamka katika ulimwengu wake, na hiyo ni kwa mujibu wa elimu yake na dunia yake, na kuna muonyaji wa jinsi yake, na vyenyewe kwetu sisi ni Umma uliofadhilishwa na Mwenyezi Mungu wao kwa wao” ([65]).

Na kwa upande huo huo baadhi ya wenye maarifa miongoni mwa Masheikh wa kisufi walikuwa wana mazingatio katika baadhi ya vitu vya ulimwengu huu miongoni mwa vitu visivyo na uhai na vingine miongoni wa wanyama wasio na akili, wakafahamu kupitia matendo yao maana zinazomuweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumsaidia kwenye mwenendo wake na kuinua nafsi yake na kuitakasa na kufanya matendo mazuri kwa tabia zake, na akaitwa kwa mfano Sheikh mwenye tabia hizi au zile, kwa upande wa kila kitendo katika vitendo vya Mwenyezi Mungu Mtukufu Sheikh mkamilifu mwenye kuongoza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ina maanisha maana hii kauli yake Mola Mtukufu kwa upande wa mtoto wa Nabii Adam ambaye alimuuwa ndugu yake:

{Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anaye fukua katika ardhi ili amuoneshe namna ya kumsitiri ndugu yake} Al-Maidah: 31. Na imepokewa Hadithi na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema: “Neno la hekima ni lenye kutafutwa na Muumini, popote alipatapo basi ni mwenye haki nalo”. Tamko lake: “Lenye kutafutwa na Muumini” kwa maana: Bado anaendelea kulitafuta kama mtu anavyotafuta kilichompotea, na kauli yake: “Popote atakapolipata ni mwenye haki nalo” kwa maana: Kuifanyia kazi na kuifuata, kama vile aliyepotelewa haangalii ubaya wa aliyemletea ([66]).

Na katika yanayoonesha tabia ya wema kwa upande wa vitu visivyo na uhai ni yafuatayo:

Kuvilinda ikiwa ni vyenye thamani, nayo ni katika wema, asili ni haramu kwa mwanadamu kuharibu kile chenye thamani ya kifedha, imepokewa Hadithi na Malik katika kitabu cha Al-Muutwii kutoka kwa Abi Huraira R.A Mtume S.A.W amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu anachukia kupoteza mali”.

Mtume S.A.W kwa ujumla amekataza kulaani, na akakanusha Muislamu kusifika na sifa hii, imepokewa Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Ibn Omar R.A Mtume S.A.W amesema: “Muumini hawi mwingi wa kulaani”, na hii inakusanya kila kitu mpaka vitu visivyo na uhai, imepokewa pia Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Ibn Abbas R.A kulikuwa na mtu mbele ya Mtume S.A.W aliulaani upepo, Mtume S.A.W akasema:

“Usiulaani upepo kwani wenyewe ni wenye kuamrishwa, na mwenye kulaani kitu kisichostahiki, laana hurejeshwa kwake”.

Mtume S.A.W alikuwa akitoa hotuba akiwa kwenye kigogo, ilipotengenezwa mimbari akakiacha kigogo na kwenda kwenye mimbari, kigogo kililia kwa uchungu kwa kuachwa na Mtume S.A.W. Imepokewa Hadithi na Ibn Maja kutoka kwa Anas R.A Mtume S.A.W alikwenda kwenye kigogo na kukikumbatia kikanyamaza, akasema: “Lau nisingekikumbatia kingelia mpaka siku ya Kiyama”. Na hii ni katika miujiza ya Mtume S.A.W.

Haya ndio ya mwisho tuliyotaka kuyaandika kwa ufupi mbali kabisa na kukusudia kufika mwisho na kukithirisha nukuu katika sherehe, hilo linapelekea kuangaliwa na watafiti wa mambo ya dini kwa ujumla kutukuza Sharia hii Tukufu, yenyewe haijaja ili kuleta uharibifu au kuuwa kiholela na kumwaga damu za watu wasio na hatia au kuisambaza kwa nguvu, bali imekuja ili kujenga ulimwengu huu na kueneza roho ya mambo ya kheiri na wema, haikuwa isipokuwa ni rehma kwa walimwengu, na huenda inavuta mtazamo wa waandishi wa masuala ya Sharia ya Kiislamu hasa katika kuonesha pande za kimaadili katika hukumu za Kiislamu ndani ya vitabu vyao kadiri itakavyowezekana.

Na mwisho wa wito wetu ni kusema shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mlezi wa Walimwengu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

[1] Kitabu cha Taaji Al-Aruus cha Zaidy 31/510.

[2] Angalia hilo kitabu cha: Ghayatul-Wusuul cha Sheikh Zakaria Al-Ansar ukurasa wa 6, 7. Na kitabu cha Misingi ya Sharia cha Sheikh Zuhair 1/69 – 71.

[3] Kitabu cha Al-Alawiih At-Tawdhiih 1/21.

[4] Angalia hili katika kitabu cha: Taajul-Aruus 25/257, 258, na kitabu cha Taarifaat cha Jarjany ukurasa wa 101, tafasiri ya Qurtwuby 18/227, tafasiri ya Tahriir wa Tanwiir 18/171, 172.

[5] Angalia kitabu cha: Taisiir sherehe ya Jaamii Swaghiir 1/362, na kitabu cha Mirqaatul-Mafaatiih 8/3183.

[6] Kitabu cha Al-Jaamii Li Ahkaami Al-Qurani 18/117.

[7] Angalia kitabu cha: Faidhul-Qadiir 5/170.

[8] Kitabu cha Bahjatul-Majaalis 2/600.

[9] Angalia kitabu cha: Abkaar Al-Afkaar cha Al-Aamadi 2/121.

[10] Kitabu cha Bahrul-Muhiitwu cha Zarkashy1/188.

[11] Kitabu cha: At-Talwiih ala Tawdhiih 2/244.

[12] Kitabu cha Ghayatul-Wusuuli ukurasa wa 7.

[13] Kitabu cha: Minhaaj Al-Wusuuli cha Baidhawi ukurasa wa 13.

[14] Angalia: Kitabu cha Jam’u Al-Jawaamii sherehe ya Al-Mahilly 1/292. 293.

[15] Kitabu cha Usuulil-Fiqhi cha Khilaaf ukurasa wa 32.

[16] Kitabu cha Jam’u Al-Jawamii, sherehe ya Al-Mahallah 2/210/ 211.

[17] Angalia kitabu cha: Usuulul-Fiqhi cha Khilaaf ukurasa wa 52.

[18] Imepokewa na Abdu Ibn Hamid katika Musnadi yake. Iliyochaguliwa namba 783. Na akasema Baihaqy: Hadithi hii ni maarufu na upokezi wake ni dhaifu haujathibiti katika upokezi huu. Mwenyezi Mungu Anajua zaidi.

[19] Tafasiri ya An-Nasafi 2/119.

[20] Kitabu cha Dustuur Al-Akhlaaq fii Al-Qurani cha Sheikh Darraz ukurasa wa 50.

[21] Kamusi ya Al-Muhiitw ukurasa wa 1189.

[22] Kitabu cha: Mufradati fii Ghariibi Al-Qurani ukurasa wa 231.

[23] Kitabu cha Taaji Al-Aruus 34/421.

[24] Kitabu cha Ruuh Al-Maani 15/29.

[25] Kitabu cha Maqswad Al-Aasy ukurasa wa 45, 46.

[26] Kitabu cha: Uddatul-Swabiriin ukurasa wa 48.

[27] Kitabu cha: Shajaratul-Maarif wal Al-Ahwaal ukurasa wa 22.

[28] Kitabu cha: Shajaratul-Maarif wal Al-Ahwaal ukurasa wa 40.

[29] Kitabu cha: Jaamii Al-Uluum wal Hikam 2/380.

[30] Kitabu cha Aqdul-Madhluum cha Qurafi 1/351, pia kitabu cha Tanqiihul-Mafhuum ukurasa wa 84, At-Tahjiir Sherhu Swaghiir cha Mardawey 5/2350.

[31] Kitabu cha Bahrul-Muhiitw 4/84, Sherhu Kaukabu Al-Muniir 3/125.

[32] Kitabu cha: Al-Ihsaan fii dhaui Al-Kitabu wa Sunna, ukurasa wa 106.

[33] Angalia katika kamusi elezo ya: Nadhratun-Naiim 2/76: 88.

[34] Kitabu cha Hashiyatu Al-Adawy sherehe ya Al-Kharshi ya Mukhtasari Khalil 2/168.

[35] Kitabu cha Ihaau Uluumi Diin 1/236.

[36] Kitabu cha Jaamii Al-Uluumi wal-Hikami 2/139. Na kitabu cha Fathul-Baary 4/104.

[37] Tafasiri ya Al-Baidhawi 2/28.

[38] Tafasiri ya An-Nasafi 3/578.

[39] Tafasiri ya Imamu Razy: 16/78.

[40] Kitabu cha Al-Bahru Raaiq 2/352.

[41] Sherehe ya Imamu Bukhary cha Ibn Batwal 6/211.

[42] Kitabu cha Al-Kulliyaat 159.

[43] Angalia: Tafasiri ya Baidhawi 1/163, tafasiri ya An-Nasafy 1/226 na tafasiri ya Al-Jalalain ukurasa wa 62.

[44] Kitabu cha Asnaa Al-Matwalib 2/ 37, 38.

[45] Sherehe ya Imamu An-Nawawi ya kitabu cha Sahihi Muslimu 11/42.

[46] Tafasiri ya An-Nasafi 1/344.

[47] Angalia kitabu cha Mirqaatul Mafaatiih 5/2115

[48] Kitabu cha Maalim Sunan 2/280.

[49] Angalia tafasiri ya Al-BAidhawi 1/122

[50] Tafasiri ya Al-BAidhawi 1/321.

[51] Kitabu cha Historia ya Ibn Khalduun.

[52] Angalia: Tafasiri ya Baidhawy 1/127.

[53] Kitabu cha Ruuh Al-Maany 6/48.

[54] Kitabu cha Ahkaami Al-Qurani 2/418.

[55] Kitabu cha Aunu Al-Maabud 7/312.

[56] Kitabu cha Maalim As-Sunan 2/317.

[57] Kitabu cha Fat’hul Baary 10/441

[58] Sherehe ya Imamu An-Nawawy ya kitabu cha Sahihi Muslimu 2/17.

[59] Sherehe ya Imamu An-Nawawi ya Sahihi Muslimu 14/240.

[60] Kitabu cha Majmuui 2/585.

[61] Fat’wa ya Ofisi ya Mufti kuhusu Waqfu kwa upande wa maasi, iliyopewa namba 1809 ya mwaka 2008.

[62] Imepokewa na Muslimu katika kitabu cha mambo bora – mlango wa nasaba ya Mtume S.A.W na kujisalimisha jiwe kwa Mtume kabla ya kupewa Utume, kutoka kwa Jabir Ibn Samura, amesema: Mtume S.A.W amesema:

“Hakika Makka kuna jiwe lilikuwa linanisalimia wakati wakati wa kupewa Utume, hakika mimi ninalifahamu hivi sasa”.

[63] Imepokewa na Imamu Bukhary katika kitabu cha jihadi – mlango wa ubora wa huduma vitani – kutoka kwa Anas Ibn Maliki R.A

[64] Imepokewa na Imamu Bukhary katika kitabu cha Hadithi za Manabii – mlango wa habari ya Al-Khidhr na Nabii Musa A.S, na Imamu Musiimu katika kitabu cha – Mambo bora – mlango wa miongoni mwa mambo bora ya Nabii Musa A.S kutoka kwa Abi Huraira R.A

[65] Kitabu cha “Ruuhul-Qudus fii Muhaasabati Nafsi” ukurasa wa 154.

[66] Kitabu cha Taisiir Sherehe ya kitabu cha Al-Jaamii As-Swaghiir 2/227.

Share this:

Related Fatwas