Makhawariji ndio ni kikundi kibaya zaidi katika historia ya Kiislamu
Question
Kwa nini Makhawariji walikuwa kikundi kibaya zaidi katika historia ya Kiislamu?
Answer
Miongoni mwa maafa yaliyoupata umma huu baada ya kuondoka Mtume, (S.A.W), ni kudhihiri kwa kikundi cha Khariji, ambacho kiliwatangaza kwamba Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), ni makafiri na kuwahalilisha damu zao, na wakageuza tofauti ya rai katika kupigana na kuruhusu damu na heshima, na walimwaga damu ya wasio na hatia, na wakawatangaza Waislamu wa tauhidi kuwa ni makafiri, kiasi kwamba wamemtangaza kuwa Ali Ibn Abi Talib (R.A) ni Imamu wa makafiri, wakamwua, naye ndiye Khalifa aliyeongoka, ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alimwambia: “Wewe kwangu mimi ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa hakuna nabii baada yangu.”
Hatari mojawapo ya kikundi hiki ni kuwa walikuwa wakijifanya ibada nyingi kwa kuswali na kufunga, basi wajinga wanaweza kudanganyika kwa hayo na kudhani kuwa wako kwenye haki, na ndio maana Mtume wa Mwenyezi Mungu. (S.A.W), alituonya dhidi yao. Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Ali Ibn Abi Talib (R.A) kwamba Mtume (S.A.W)alisema: Watatokea watu katika zama za mwisho wajinga Wasio na busara; au akasema ni chipukizi watakuwa wakisema kauli nzuri yao ya viumbe (lakini) imani yao haivuuki kwenye koo zao (hawana imani), wanatoka katika dini kama mshale unavyotoka katika kiwindwa, basi popote mnapowakuta wauweni, kwani katika kuwaua wao kuna ujira mkubwa Siku ya Kiyama kwa atayewaua”.