Kugawanyika ulimwengu kati ya nchi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kugawanyika ulimwengu kati ya nchi ya amani na nchi ya vita, na dalili ya hilo.

Question

Nini maana ya nchi ya amani na nchi ya vita katika Uislamu, na je kuna dalili ndani ya Qur`ani au Sunna ya mgawanyo huo?

Answer

Imani ya vikundi vingi vya ukufurishaji na ugaidi inasimama kwenye ufahamu potofu wa hukumu nyingi za maana mbalimbali, miongoni mwazo ni maana ya nchi ya vita na nchi ya Uislamu, nao ni uelewa wa masuala yenye kufungamana yenyewe kwa yenyewe, kuugawa ulimwengu kati ya nchi ya amani na nchi ya vita kunaendana na hukumu zinazohusiana na kuhama pamoja na jihadi.

Maudhui ya kugawa nchi za ulimwengu kati ya nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu ni moja ya maudhui muhimu yenye asili ya kisiasa katika Fiqhi kwa kufungamana kwake na mtazamo wa Kiislamu kwa ulimwengu na kufungamana kwake na masuala ya jihadi na hukumu ya wafuasi wachache wa dini kwa sababu ndio msingi wa taswira ya Fiqhi ya mahusiano ya kimataifa.

Ndani ya Qur`ani Tukufu au Sunna Takatifu hakuna kinachoeleza au kuashiria mgawanyiko wa nchi za dunia kwa mujibu wa imani ukafiri au vita na amani, ni kwa sababu mgawanyiko huu ni mtazamo wa kifiqhi kwenye mahusiano ambayo yalikuwa kati ya Waislamu na wasio Waislamu, ambapo mara nyingi vita ndio hukumu pekee ya jambo hilo panapo kuwa hakuna makubaliano, ni mgawanyo unaosimamia msingi wa matukio na wala si msingi wa Sharia, wala kusudio lake halikuwa kuufanya ulimwengu kuwa chini ya hukumu ya dola mbili au makundi mawili ya kisiasa, kundi moja linakusanya nchi za Kiislamu zinaendeshwa na dola moja, na kundi lingine linakusanya nchi za kigeni zinaendeshwa na dola nyingine, bali ni mgawanyo kwa mujibu wa kupatikana kwa usalama na amani kwa Waislamu katika nchi yao, na kuwepo hali ya hofu na uadui kwa Waislamu nje ya nchi yao.

Share this:

Related Fatwas