Uhusiano kati ya maneno ya fitina n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhusiano kati ya maneno ya fitina na Jihadi.

Question

Upi ukweli wa maneno ya fitina? Na yapi mahusiano yake na Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?

Answer

Ni maneno yanayotumiwa na vikundi pamoja na mitandao ya kigaidi ambayo yanajificha kwenye vazi la Uislamu na maana zake nzuri wakati wanayoyafanya ni ukiukaji na umwagaji damu iliyozuiliwa kumwagwa, nayo ni Jihadi ya maneno yasiyo sahihi yanatokana na ufahamu mbaya, na hivyo ni kuwa wanayoyafanya ni “Maneno ya fitina” ambayo Mwenyezi Mungu Ametaja katika kauli yake: {Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitina katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu * Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa * Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu} Al-Ahzaab: 60 – 62. Nayo ni maneno yenye uelewa mbaya (kwa wenye msimamo mkali) ambao una maanisha kuleta fitika na migongano pamoja na hali za wasi wasi kwa kuhalalisha damu na mali kati ya wana jamii moja chini ya madai tofauti, miongoni mwayo: Kukufurisha Kiongozi au nchi au kundi fulani la watu, pia kuhalalisha damu za Waislamu chini ya madai kuamrisha mema na kukataza maovu, au kuhalalisha damu za wasio Waislamu ndani ya nchi zao au wale ambao wameingia ndani ya nchi za Waislamu kwa madai ya kuwa nchi yao inapigana vita na Uislamu…na yasiyokuwa madai hayo ya uongo na kuleta fitina, na ambayo baadhi yake yalikuwa ndio sababu ya kuibuka vikundi vya khawariji wakati wa zama za Masahaba na waliokuja baada yao na wakitoa hoja ya uharibifu wao duniani na kumwaga kwao damu iliyo haramu kumwagwa.

Share this:

Related Fatwas