Istilahi ya nchi ya ukafiri na nchi ya Uislamu
Question
Je, istilahi za nchi ya ukafiri na nchi ya Uislamu bado zatumika? Ni nini mazingira ya kihistoria yaliyochangia istilahi hiyo kujitokeza.
Answer
Hapana haja ya kuendelea kutumia istilahi ya nchi ya kikafiri na nchi ya Kiislamu (Darul-Kufr na Darul-Islam) katika zama hii, hasa katika hali ya kufunga mikataba na mahusiano ya kimataifa ya kisasa ambayo ilikubaliwa na nchi zote duniani, kutoendelea kutumia istilahi kama hiyo kumechangia kujitokeza istialahi mpya kama vile; istilahi ya nchi ya kiraia ya kisasa, dhana ya uzalendo ambapo kuwabagua wananchi katika haki na wajibu kulingana na dini, kabila, rangi, nasaba ikawa uhalifu unaostahiki adhabu katika Sheria za nchi zote duniani, kinyume na hali ilivyokuwa tangu karne moja, ambapo ubaguzi ulikuwa msingi mojawapo ya misingi ya utamaduni wa ulimwengu mzima, jambo lililowasukuma Wataalamu wa Fiqhi kuunda istilahi kama vile; Darul-Kufr na Darul-Islamu - kukidhi mahitaji ya zama hizo -, ilhali Uislamu ulisisitiza katika matini nyingi za kisheria zilizopo katika Qur'ani na Sunna za Mtume (S.A.W.) kupinga na kukataa ubaguzi huu, kwa hiyo Wanazuoni Waislamu walikuwa wa mwanzo kukaribisha maazimio, mikataba na istilahi hizo mara moja tu baada ya kujitokeza.