Mchango wa usufi katika kutengeneza...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mchango wa usufi katika kutengeneza haiba ya Kiislamu ya ukati na kati

Question

Ni upi Mchango wa usufi katika kutengeneza haiba ya Kiislamu ya ukati na kati?

Answer

Usufi ni cheo cha wema ambao Mtume S.A.W. ameufafanua katika kauli yake: “Ni kumwabudu Mwenyezi Mungu kama kwamba unamwona, ikiwa humwoni, basi yeye Anakuona” [Imekubaliwa na wote], na nadharia za elimu hii zimetofautiana kwa Wanazuoni mpaka zimevuka nadharia mia mbili, na kwa kuangalia tunakuta nadharia zao zipo katika maana mbili; ya kwanza: kushindana na nafsi kwa mujibu wa Sharia, hali hii inaleta usafi wa juu wa roho, na ya pili: Kushuhuduia ukweli, na ukweli kwa mabwana wakubwa wa Kisufi ni: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na miongoni mwa maneno yao mazuri ni: “Kiasi cha kujitoa ndiyo kunapatikana ushuhuda”, na neno lao: “Usufi ni tabia, aliyekuzidi kitabia amekuzidi katika usufi”, na miongoni mwa masharti ya masufi ni kupatikana sheikh mlezi ambaye anasimamia kuwalea Muridi (mfuasi wa Kisufi) na kumwongoza katika njia ya Mola wake Mtukufu, na miongoni mwa sifa za Usufi ni kwamba umechukuliwa kwa Sanadi mpaka kwa Mtume S.A.W. na njia hii akiipita Muislamu inamlinda na fikra za itikadi kali ambazo hazikujengwa isipokuwa kwa tabia mbaya kama kiburi, dhana mbaya kwa viumbe, kuingilia yasiyowahusu na kujishughulisha na Dunia.

Share this:

Related Fatwas