Dhana sahihi ya kurejelea Sheria ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhana sahihi ya kurejelea Sheria ya kiislamu katika hukumu

Question

Ni ipi dhana sahihi ya kurejelea Sheria ya kiislamu katika hukumu, na kwa namna gani makundi ya kigaidi yalichafua dhana hiyo?

Answer

Kwa hakika dhana sahihi ya kurejelea Sheria ya kiislamu katika hukumu ni kukubali hukumu itokanayo na Sheria ya kiislamu na kutegemea Sheria kuwa chanzo cha Sheria, kwa kuwa hukumu za Sheria ya Kiislamu ndizo hukumu za Mwenyezi Mungu (S.W.), lakini makundi ya kigaidi yalichezea dhana hiyo na kupotosha maana yake ya kweli, wakaelewa Qur`ani na Sunna kimakosa, na kubuni mbinu isiyo sahihi inayotegemea ule uelewa usio sahihi, wakaifanya mbinu hiyo sawa sawa na Sheria ya Kiislamu, kwa hiyo wanaona kuwa yeyote anayekataa mbinu yao hiyo huwa anakataa Sheria na kurejelea hukumu na Sheria za Taghuti, pia wanasisitiza kuwa kutekeleza mbinu yao wanayoizingatia ni Sheria ya Mwenyezi Mungu ni sharti mojawapo ya masharti ya Imani sahihi, na kuwa anayekataa sheria hiyo kuwa amekufuru kwa Mwenyezi Mungu (S.W.).

Kwa hakika, hukumu za Sheria ni sehemu mbili kuu; ya kwanza ni zile hukumu zilizokubaliwa na wanazuoni wote wa Fiqhi katika zama zote na mahali pote nayo ni sehemu inayoitwa Sheria ya Kiislamu, pengine sehemu ya pili ni zile hukumu ambazo wanazuoni hawakukubaliana kuhusu hatima yake na katika hali hii Muislamu huruhusiwa kurejelea rai yoyote kati ya rai tofauti zilizotolewa na wanazuoni wa Fiqhi huwa inaambatana na Sheria na kuwa sehemu mojawapo ya sehemu zake, pamoja na kuwa kutotekeleza hukumu za Mwenyezi Mungu ni dhambi isiyosababisha kumhukumia mtu kuwa amekufuru au ameritadi, kwa mujibu wa maoni ya wataalamu wa Fiqhi.

Share this:

Related Fatwas