Mfumo sahihi wa kuboresha namna ya kufikisha hotuba ya kidini
Question
Ni nini makusudio ya kuboresha hotuba za kidini? Na ni mfumo gani ulio sahihi kwa kufanya hilo?
Answer
Maana ya kuboresha hotuba za kidini ni kurejelea moja kwa moja vyanzo vya asili vya dini, ambavyo ni Qur`ani Tukufu na Sunna za Mtume (S.A.W), pamoja na kupambanua hotuba za kidini na yale yaliyochanganywa nayo katika siku za hivi karibuni miongoni mwa tamaduni, mila na desturi zisizoambatana na dini hata kidogo, kama vile; kumdharau mwanamke ambayo ni tabia isiyo ya kiislamu, iliyomwekea mwanamke vikwazo na vizuizi visivyokuwepo katika Qur`ani na Sunna, bali huenda vinapinga yaliyokuja katika vyanzo hivi viwili vya sheria ya Kiislamu mfano wa kumkataza mwanamke kutoka nyumbani na kufanya kazi au kutekeleza majukumu yake ya kisiasa na ya kijamii, pia, maelezo yanayofungamana na uhusiano wa Muislamu kwa asiye Muislamu, ule uhusiano uliochafuliwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya kutoelewa vema msimamo wa Uislamu kuhusu jambo hilo, ambapo Uislamu huhimiza kuishi pamoja kwa amani na kushirikiana baina ya Waislamu na wasio Waislamu si kupigana na kuchukiana, ama kuhusu mbinu sahihi ya kuboresha namna ya kufikisha hotuba ya kidini, basi ni kurejelea Qur`ani Tukufu na kuongoka kwa mafunzo yake, Mweneyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi} [An-Nisaa: 174], pamoja na kutambua hekima Alizotuongoza Mwenyezi Mungu (S.W.), kama vile; tabia ya uwiano baina ya wanadamu, kujuana, na kukamilishana, na kuzingatia kanuni kuu mfano wa: "Hukumu ya mambo hupimwa kwa malengo yake", "Madhara huondolewa", "Dharura hukadiriwa kwa kiasi chake tu", "Kuzingatia ada za watu" pamoja na kuhakikisha kutekeleza malengo Makuu ya Sheria ya Kiislamu kama: kuilinda nafsi, akili, dini, mali, heshima na utukufu wa mwanadamu.