Faini na Malipo ya fidia ya kuahirisha kulipa deni
Question
Ni ipi hukumu ya faini na fidia ya fedha kwa sababu ya kutolipa deni kwa wakati?
Answer
Faini zinazopitishwa na mamlaka ya kisheria na kuhukumiwa mwenye kudaiwa deni aliyechelewa kulipa kwa wakati si riba bali ni fidia anapata mwenye deni kumtuliza kuchelewa kupata deni lake, na ni sababu ya kuhifadhi mali za watu, zisiliwe kwa batili na wale wenye tabia ya uchoyo, udanganyifu na uwongo, Hadithi sahihi Mtume (S.A.W.) alisema: “Yeyote anayechukua mali ya watu akiwa na nia ya kuyarudisha, basi Mwenyezi Mungu Anamsaidia kuyarudisha, lakini anayechukua akiwa na nia ya kuyapoteza, basi Mwenyezi Mungu Atampoteza”, naye Imamu Bukhary alisimulia kutoka kwa Abu Hurairah (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Hakika, mwenye mali kuchelewa kulipa deni humwajibishia aadhibiwe na kuvunjwa heshima yake”; yaani: akiwa mtu anaye mali na kuchelewa kulipa deni lake kwa makusudi na kupoteza haki za wengine ni dhuluma inayomruhusu mtawala au hakimu kumhukumu kufungwa kwa kumwadhibu.