Dalili ya kisheria na ya kiakili ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Dalili ya kisheria na ya kiakili ya kujinasua na Daishi

Question

Ni ipi dalili ya kisheria na ya kiakili ya kujinasua na Daishi?

Answer

Hali ya kujiunga na Daishi ni marufuku kwa mujibu wa sheria, na kuibadilisha ni dharura ya kisheria na ya kibusara. Daishi ni kundi la kigaidi lililo nje ya mafundisho ya Uislamu.linaua Waislamu na kuuawa, huku viongozi wao wakifurahia maisha ya anasa na kuepukana na mauti. Basi ni hekima ya aina  gani hiyo ya kuendelea kuishi na ni malipo gani yanayopatikana zaidi ya kupoteza dunia na akhera?

Na hakuna kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu zaidi ya damu na kuimwaga isivyo haki, wanachofanya Daishi katika kuua, kukamata na kuchukua pesa za watu kinyume cha sheria ni ukiukaji wa makatazo ya Mwenyezi Mungu na kukiuka njia ya ukweli kwa jina la dini, na dini iko mbali nao.

Mtume (S.A.W) anasema: “Madhambi makubwa zaidi ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuua nafsi.” Wanaua Waislamu na wala hawatofautishi baina ya mwanamume na mwanamke, mzee au kijana, wanaiharibu ardhi kwa thamani ya kupita, na dhana potofu. Mtume amesema (S.A.W): “Na mwenye kuuasi umma wangu, akawapiga watu wema na waovu, wala hawaepukiki waumini wake, na wala hatimizi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu wala mimi si pamoja naye.”

- Yeyote aliyejihusisha na kundi hili la kigaidi la umwagaji damu ametoka patupu, na amepata hasara , na ameangamia, na hufa kifo cha kijahiliya, kwa mujibu wa Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ((S.A.W): “Yeyote anayeuawa chini ya bendera ya ujinga, akiiulingania ushabiki, au kuunga mkono ushabiki, basi mauaji yake ni ya kijahiliya.”

Share this:

Related Fatwas