Hukumu za Jihadi katika Fiqhi ya ki...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu za Jihadi katika Fiqhi ya kiislamu na maazimio na mikataba ya kimataifa

Question

Je, kutofautiana kwa baadhi ya hukumu za Jihadi katika Fiqhi ya kiislamu kulingana na maazimio na mikataba ya kimataifa huzifuta hukumu zile? Na nini msingi wa hayo?

Answer

Kwa hakika kutofautiana kwa baadhi ya hukumu za Jihadi kati ya Fiqhi ya kiislamu na maazimio na mikataba ya kimataifa haiathirii ahadi hizo kwa namna yoyote, kwani hukumu zile zimetokana na jitihada za Wataalamu kulingana na zama na hali halisi ambapo hukumu zile zimetolewa, kwa hiyo hukumu hizo hubadilika kufuatana na kubadilika kwa zama na hali halisi ya mambo, hivyo tunaona Wanavyuoni wa kisasa hawakupinga maazimio na mikataba hiyo, bali waliikubali na kuiunga mkono, kinyume na wale waliotegemea vitabu katika jitihada za kupata elimu pasipo na kujifunza moja kwa moja kutoka kwa sheikh, ambapo baadhi ya watu hawa hukosa hukumu na mtazamo ulio sahihi, hivyo inasemekana kuwa; yeyote anayepata elimu yake kutoka katika kitabu tu basi makosa yake huwa mengi zaidi kuliko mafanikio yake.

Msingi katika suala la kuathiriwa kwa maazimio na mikataba mpaka ihukumiwe kwa upotofu ni kutoendana kwake na hukumu ya kisheria iliyo thabiti na kukubaliwa na Wanafiqhi wote, hakuna katika hukumu za Jihadi hukumu iliyo thabiti na ya hakika isipokuwa sababu za msingi za kutunga Sheria ya Jihadi zilizotajwa wazi katika Qur`ani na Sunna kwa lengo la kuitetea nafsi, ama hukumu zake ndogo ndogo, basi hutofautiana kutokana na mabadiliko ya enzi, wakati, hali ya Waislamu na hali ya maadui wao.

Share this:

Related Fatwas