Hukumu ya kuharibika kwa bidhaa baa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuharibika kwa bidhaa baada kumaliza ununuzi wake na kuiacha kwa muuzaji aiweka amana

Question

Ni ipi hukumu ya kuharibika kwa bidhaa baada kumaliza ununuzi wake na kuiacha kwa muuzaji aiweka amana?

Answer

Akija mtu akanunua bidhaa fulani na kulipa bei yake lakini bila ya kukabidhiwa bidhaa hiyo, bali aliiweka kwa muuzaji mpaka yule mnunuzi arudi tena baada ya kumaliza shughuli kadhaa, ni miamala miwili nayo ni:

Mkataba sahihi ya kuuza unao nguzo na mashsarti kamili, ambao kwa mujibu wake mnunuzi ameimiliki bidhaa ikawa mkononi mwake na kuwa na haki ya kuifanyia atakalo.

Amana (Wadia'a) isiyo na gharama ya kuhifadhi, nayo ni mkataba wa kumpa mwingine ambaye hapa ni muuzaji haki ya kuhifadhi mali ya mnunuzi kwa njia ya kujitolea, nao ni mkataba unaoruhusiwa, ambapo ni amana na mwenye kupewa haki ya kuhifadhi hiyo amana ni mtu anayeaminiwa, yaani; anatakiwa kufanya juhudi zake zote za kuilinda na kuhifadhi mali hiyo, wala hatakiwi kulipa fidia au gharama yoyote ikiharibika au kuibiwa isipokuwa akifanya uzembe kimakusudi au kuiharibu mwenyewe, amana hiyo ikiharibika wakati ambapo iko mkononi mwa huyu mtu anayepewa jukumu la kuihifadhi hana gharama yoyote sawa ikiharibika kwa sababu ambayo inaepukakana au la, hali hii ni tofauti na kuharibika kwa amana (bidhaa) inayoshikiliwa na mtu anayepewa kiasi cha fedha kulingana na kazi hilo, basi amana ikiharibika kwa sababu ya jambo linaloweza kuepukana nayo kama vile; wizi basi analipa thamani yake au kuleta badala yake, kinyume na ikiharibika kwa jambo lisiloweza kuepukana nayo, basi hana kitu, na wakikubaliana kitu basi hamna shida.   

Share this:

Related Fatwas