Hukumu ya kutamka ibara ya: "Mungu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kutamka ibara ya: "Mungu Amemkumbuka" kwa kuashiria aliyefariki

Question

Ni ipi hukumu ya kusema: "Mungu Amemkumbuka" kwa kuashiria kifo cha mtu?

Answer

Wamisri wana msemo kwa mtu aliyeulizwa kuhusu aliyekufa bila yeye kujua kuhusu kifo chake ibara waisemayo "Mungu Amemkumbuka" kwa kueleza kuwa mtu mmoja amefariki lakini mmoja wa wanaozungumza tukio hilo hakuwa anajua taarifa ya msiba, hilo ndilo lililoenea baina ya wamisri ambapo mara tu mtu  anaposikia ibara hii anajua kuwa mtu unayemwulizia ameshafariki, kisharia ibara hii inaruhusiwa, wala haijuzu kumtuhumu anayeisema au kumfikiria vibaya kwa kufafanua kwa maana yake ya jumla inayomaanisha kuwa Mwenyezi Mungu inawezekana kuwa Amesahau hapo kabla halafu Anakumbuka, lakini kinyume na hayo Mwenyezi Mungu Hasahau, inapaswa kufafanua ibara hiyo kwa maana isiyo dhahiri iliyo nzuri nayo ni kwamba wanaosema hayo wanamwombea marehemu apate rehema ya Mwenyezi Mungu na kwamba ametoka dunia yenye mateso na mashaka kwenda kwenye pepo ya Mwenyezi Mungu yenye upana na rehema baada ya kifo chake kwa ukarimu wake Mwenyezi Mungu, pia, ibara hiyo huashiria kuwa kifo ni raha kwa muumini kutokana na mateso ya dunia na mahangaiko yake, na haya yote ni maana na maelezo mazuri kwa ibara hiyo, kutokana na yaliyokuja katika matini za kisaria na kwa mujibu wa maelezo ya Wamisri wenyewe.

Share this:

Related Fatwas