Ruhusa ya Imamu au Rais wa nchi kat...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ruhusa ya Imamu au Rais wa nchi katika Jihadi

Question

Je, ruhusa ya imamu au Rais wa nchi ni sharti katika Jihadi? Na kwa kiasi gani hayo ni hatari kusema kuwa ruhusa hiyo si sharti?

Answer

kwa hakika, kuomba ruhusa kutoka kwa Imamu au Rais wa nchi ni sharti mojawapo masharti ya Jihadi, jambo lililo wazi, halina haja ya kuongea sana, Qur`ani Tukufu imesimuliwa kuwa kundi la watu kutoka banu Isael walikuwa wakitaka kuanza Jihadi wakaanza kwa kuomba kuwepo wa Imamu ambaye atawaongoza katika vita hiyo, Mwenyezi Mungu Amesema: {Hukuwaona watukufu katika Wana wa Israel baada ya Musa, walipo mwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu?} [Al-Baqarah: 246], wataalamu wa zamani na wa kisasa walikubaliana kuwa uamuzi kuanza Jihadi kwa umma ulikuwa wa Mtume (S.A.W.) hasa kwa kuwa ni Imamu wa Waislamu na anayewakilisha baada ya kifo chake Mtawala, na kwamba Waislamu wanapaswa kuwajibika kwa uamuzi huu sawa sawa na mambo na maaelekezo mengini, hivyo, Imamu au anayemwakilisha ni wa pekee ndiye anaye haki na mamlaka ya kusaini mikataba ya amani kwa mujibu wa mfumo wa nchi ya kiraia, pia yeye pekee anaye mamlaka ya kutangaza vita, hivyo, kutomshauri Rais katika vita ni ukiukaji na kosa kubwa linalostahiki adhabu, kwa kuwa jambo kama hilo huenda kupelekea hatari kubwa mno.

Share this:

Related Fatwas