Uhalifu uliofanywa na kundi la Dais...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhalifu uliofanywa na kundi la Daish

Question

Uhalifu gani uliofanywa na kundi la Daish?

Answer

Kundi la kigaidi la Daish limefanya ukiukaji mkubwa wa kisheria, ingawa kundi hili la umwagaji damu lilitokana na madai ya kutekelezwa kwa sheria ya Kiislamu, ambayo inadaiwa kuwa haitekelezwi, na kati ya ukiukwaji huo: kuwalazimisha wasio Waislamu kuingia Uislamu kulingana na sheria zao na mbinu wao potovu, au kulipa kodi, miongoni mwa uhalifu huo, matumizi ya mateso na tishio la kuua ili kuwalazimisha watu kutoa ahadi ya utii kwa kiongozi wao, miongoni mwa uhalifu huo pia ni ubadhirifu, uasherati na majigambo ya kuua, na wanarekodi kanda za video kwa hilo na kuzieneza kwenye mtandao, na Sharia tukufu ilikataza yote hayo, ikiwa ni pamoja na kuwazuia kufundisha historia na fasihi ya kitaifa au inayorejelea tamaduni au dini tofauti na mtaala wao, na kutoka kwa ukiukaji huo ni kupitishwa kwa bendera nyeusi kama nembo yao, wakidai kuwa hii ni Sunnah, na ukweli ni kwamba Mtume, (S.A.W.), hakubainisha rangi maalumu kwa ajili ya bendera yake. Miongoni mwa ukiukwaji wao ni kuzuia watu kujiunga na vyuo vya jeshi na polisi ili wanaojiunga wasiwe wafuasi wa tawala zisizofuata misimamo yao ya itikadi kali, na miongoni mwa ukiukwaji wao ni kutoruhusiwa kusoma katika Vitivo vya sheria. Hii ni kwa sababu Vitivo hivi vinafundisha sheria chanya inayopingana na Sharia, kama wanavyodai!

Share this:

Related Fatwas