Kusema Bismillah wakati wa kuanza k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusema Bismillah wakati wa kuanza kula

Question

Nini hukumu ya kusema Bismillah wakati wa kuanza kula? Nini hukumu ya aliyesahau kusema hivyo halafu amekumbuka wakati wa kula?

Answer

Kusema Bismillah wakati wa kuanza kula ni Sunna; Kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Umar Ibn Abi Salamah, (R.A), amesema: Nilikula pamoja na Mtume (S.A.W), na mkono wangu ukazunguka bakulini, akasema: “Mtaje Allah (Sema Bismillah), na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kinachokuelekea.” Imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah kwa maana yake, na Abu Daawuud.

Atakayeisahau hapo mwanzo, basi ataje anapoikumbuka, na aseme: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwanzoni mwake na mwishoni mwake”; Kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Bibi Aisha, Mama wa Waumini, (R.A), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Akila mmoja wenu ataje jina la Mwenyezi Mungu, na akisahau kulitaja hapo mwanzo, na aseme: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwanzoni mwake na mwishoni mwake.” Imepokelewa kutoka kwa Abu Daawuud.

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas