Kumsalia Mtume (S.A.W) wakati wa kuswali
Question
Nini hukumu ya kumswalia Mtume (S.A.W), wakati wa kusali?
Answer
Kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu yule anayesikia au kusoma jina lake Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) wakati wa kusali inapendekezwa kumswalia bwana wetu. Hali hii ina sifa kubwa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuhimiza kufanya hivyo. Mwenyezi Mungu alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.” [Al-Ahzab:56]. Mafakihi walio wengi wamesema inapendekezwa kwa yeyote aliyesikia jina la Mtume wetu (S.A.W) wakati wa kusali au alisoma aya ambayo jina lake (S.A.W) liko ndani, amswalie na sala yake haibatiliki kwa hayo. Kwa sababu imeamrishwa kumswalia kila linapotajwa jina lake, (S.A.W), na hilo linatokana na ujumla wa kauli yake, (S.A.W): “Mtu bakhili ni mmoja ambaye nimetajwa mbele yake wala hanisalii” (Imepokelewa kutoka kwa Ahmad).