Kumswalia Mtume S.A.W

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumswalia Mtume S.A.W

Question

Ipi hukumu ya kumswalia Mtume S.A.W kwa muundo usiopokelewa kwenye Sunna?

Answer

Kumsalia Mtume S.A.W ni jambo linalofaa kwa muundo wowote uliopokewa au haujapokewa, madam tu inaendana na nafasi yake takatifu S.A.W.

Wala yasiangaliwe yanayosemwa na baadhi muundo huu ni uzushi, amri ya Mwenyezi Mungu ya kumswalia Mtume inakusanya kuonesha utukufu wake, kutukuza nafasi yake, kuinua haiba yake na kuinua nafasi yake. Mwenyezi Mungu Amesema: 

{Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumheshimu} Al-Fathi: 9.

Kama vile Sunna za Mtume S.A.W zimekuja na amri ya wema katika kumswalia S.A.W katika kauli yake:.

“Hakika yanafikishwa kwangu majina yenu basi niswalieni vizuri”. Na Abdillah Ibn Masoud amesema:  “Pindi mnapomswalia Mtume S.A.W basi mswalieni vizuri”. 

Mola Anajua zaidi.

Share this:

Related Fatwas