Kumswalia Mtume (S.A.W)

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumswalia Mtume (S.A.W)

Question

Nini hukumu ya kumswalia Mtume (S.A.W), kwa maneno yasiyotajwa katika Sunna?

Answer

Kumswali Mtume (S.A.W), kunajuzu kwa maneno yoyote yanayotajwa au yasiyotajwa, au kutoka kwa yaliyojaribiwa. Maadamu inaendana na hadhi yake Mtukufu (S.A.W)..

Wala usizingatie yale ambayo baadhi ya watu wanayoyasema kuhusu uzushi wa maneno hayo; amri ya Mwenyezi Mungu ya kumswalia Mtume (S.A.W) ni pamoja na kuchunga kuonesha heshima yake, kuitukuza hadhi yake, na kunyanyua nafasi yake ya juu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumhishimu.” [Al-Fath: 9], kama vile Sunna ya Mtume ilitaja amri ya kumswalia Mtume(S.A.W), kwa kusema kwake: “Mnanionesha kwa majina yenu na sura zenu; Basi mswalieni kwangu vizuri.” Abdullah Ibn Masoud (R.A) amesema: “Iwapo mtamswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), basi mswalieni kwake vizuri.” Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas