Kusoma Bismillah wakati wa kula cha...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma Bismillah wakati wa kula chakula

Question

Ipi hukumu ya kusoma Bismillah wakati wa kuanza kula chakula? Na ipi hukumu ya mwenye kusahamu na akakumbuka katikati ya kula?

Answer

Kusoma Bismillah wakati wa kuanza kula chakula ni Sunna, kwa Hadithi ya Omar Ibn Abi Salama R.A amesema: Nilikula na Mtume S.A.W na mkono wangu ukitangatanga kwenye sahani, Mtume S.A.W akasema:

“Mtaje Mwenyezi Mungu, na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kilichombele yako” Imepokewa na Ibn Maja na Abu Daud.

Mwenye kusahau kuleta Bismillah mwanzoni mwa kula kwake basi ataileta pale atakapokumbuka, na atasema:

“Bismillah Awwalau wa Aakhirau” kwa Hadithi ya Bi Aisha Mama wa Waumini R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

“Pindi mmoja wenu anapokula chakula basi na alitaje jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa atasahau kulitaja jina la Mwenyezi Mungu mwanzo mwa kula kwake basi na aseme: Bismillah Awwalau wa Aakhirau” Imepokewa na Abu Daud.

Mwenyezi Mungu Anajua zaidi.

Share this:

Related Fatwas