Kusaidia utafiti wa kisayansi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusaidia utafiti wa kisayansi

Question

Je, nini hukumu ya kutumia zakat katika utafiti wa kisayansi kuhusiana na mazingira?

Answer

Kuhifadhi mazingira ni sehemu ya kuimarisha ardhi unaotakiwa katika kauli yake Mola Mtukufu: “Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo” [Hud: 61], Mtume (S.A.W) aliamuru kuhifadhiwa kwa maliasili na kuzuia uchokozi dhidi yake akisema: “Hakuna muislamu yoyote anayepanda mazao Fulani, au mti fulani alafu akatokea ndege au mnyama yoyote akala kutokana na zao hilo inakua ni sadaka yake mtu huyo” (Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari).

Muislamu anatakiwa kufuata mbinu za kisayansi katika kuijenga upya ardhi, ambayo ni pamoja na kuhifadhi mazingira na kukabiliana na uharibifu wowote unaoweza kutokea ndani yake ambao unaleta madhara kwa jamii kwa ujumla.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiweka zakat kama dhihirisho la mshikamano baina ya watu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. [At-Tawbah: 61]

Wanachuoni wana maoni kwamba kategoria hii, kama inavyojumuisha jihadi, pia inajumuisha elimu. Kwa sababu jihadi iko kwa ulimi kama ilivyo kwa mkuki, na kwa hivyo; Kutoa zaka katika utafiti wa kisayansi kuhusu mazingira na uhifadhi wake ni miongoni mwa mambo ambayo yanajuzu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.

Share this:

Related Fatwas