Kuwahifadhi Wapiganaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwahifadhi Wapiganaji

Question

Nini hukumu ya kuwahifadhi magaidi na kuwaficha ili wasionekane kwa kisingizio cha kuwasaidia jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu?

Answer

Kuwahifadhi magaidi ni moja ya madhambi makubwa ambayo wanaofanya hivyo wanastahiki laana ya  Mwenyezi Mungu, na kudai kuwa hii ni msaada katika jihadi ni uwongo mtupu dhidi ya Sharia. Wanachofanya wahalifu hawa kutokana na  uharibifu na kuua ni miongoni mwa aina kubwa za dhuluma na ufisadi ambazo Sheria ilikuja kuzizuia, na kuwapiga vita wanaofanya hivyo ikiwa hawakujiepusha na kuwadhuru raia. Kuiita jihadi si chochote ila ni ulaghai na hadaa ili ufisadi na mtikisiko huu uwalaghai wenye fikra dhaifu, na Jamii pamoja na Mataifa yote, Madhehebu na Taasisi zake lazima zisimame mbele ya madhalimu hawa wa Khawariji na kuondosha uadui wao; kila mtu kadiri ya mamlaka na uwezo wake; Sheria iliwaamrisha watu kushika mkono wa dhalimu mpaka arudi nyuma kutoka kwenye dhuluma yake, na Mtume, (S.A.W), alionya dhidi ya kuachilia dhuluma, na kuifanya hiyo inastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hii ni kwa sababu kuachilia dhuluma husababisha uhalifu na husaidia kuueneza na kuuongeza bila upinzani. Mtume (S.A.W) amesema: “Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimzuie dhuluma yake, basi Mwenyezi Mungu yuko karibu kuwapofusha na adhabu yake.” Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ahmed, Abu Dawud. , Al-Tirmidhiy, na imethibitishwa na Ibn Majah na Ibn Hibban kutoka kwa Hadithi ya Abu Bakr Al-Siddiq, (R.A).

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas