Kununua nyumba kabla ya kujengwa

Egypt's Dar Al-Ifta

Kununua nyumba kabla ya kujengwa

Question

Ipi hukumu ya kununua nyumba kabla kujengwa?

Answer

Miongoni mwa makusudio muhimu ya Sharia ya Kiislamu ni kufikiwa masilahi ya waja, na kuondoa uharibifu kwao, ambapo asili katika mashirikiano ambayo yamejengwa kwa maridhiano ni halali, pindipo tu hayatagongana na andiko la Sharia, na hilo ni kutokana na mahitaji makubwa ya watu, miongoni mwa mashirikiano haya ni makubaliano ya ujenzi, kwani washiriki ambao wanafanya kazi hii wanakubaliana ujenzi wa nyumba yenye wasifu maalumu wanayokubaliana kati ya mnunuzi na muuzaji, na wasifu huu unapelekea ndio sifa wanazokubaliana na kubainishwa wazi kwenye masharti ya mkataba, hivyo kununua nyumba kabla ya ujenzi wake hayo ndio makubaliano ya ujenzi, nayo ni katika mambo ambayo watu wanayafahamu na wanashirikiana kwayo, hivyo ni makubaliano yanayokubalika halali pindi masharti yatakapotimilika mbali na udanganyifu na kuainisha muda pamoja na thamani na namna ya kulipa ili kuzuia mvutano na tafauti masiku ya mbeleni. 

Share this:

Related Fatwas