Kufuta uso baada ya duwa.
Question
Ipi hukumu ya kufuta uso kwa mikono miwili baada ya dua ambapo kuna wanaosema kuwa huo ni uzushi unaochukiza?
Answer
Ni katika Sunna kuinua mikono miwili wakati wa duwa, na kufuta uso kwa mikono hiyo miwili baada ya duwa ndani ya swala na nje ya swala, haya ndio yaliyopitishwa na Jamhuri ya Wanachuoni.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Ametuamrisha kufanya duwa na kuahidi kujibu, Mola Amesema:
{Na Mola wenu Mlezi Amesema niombeni nitawajibu} Ghafir: 60.
Na katika Sunna ambazo zinapendeza kuzifanya wakati wa duwa ni kuinua mikono miwili, na kufuta uso kwa mikono miwili baada ya duwa ndani ya swala na nje ya swala, haya yamepitishwa na Wanachuoni juu ya kufaa kwake kwa upande wa Imamu Abu Hanifa Imamu Shafi na Imamu Hambali, kwa kauli ya Mtume S.A.W:
“Pindi mnapomuomba Mwenyezi Mungu basi muombeni kwa matumbo ya viganja vyenu, wala msimuombe kwa migongo yake, na panguseni kwa viganja hivyo nyuso zenu” Imepokewa na Hakim.