Kupangusa uso baada ya dua

Egypt's Dar Al-Ifta

Kupangusa uso baada ya dua

Question

Ni nini hukumu ya kupangusa uso kwa mikono baada ya kuomba dua, kwani wapo wanaosema kuwa huu ni uzushi usiokubalika?

Answer

Ni Sunna kunyanyua mikono wakati wa kuomba dua, na kupangusa nayo uso baada ya kuomba dua, ndani ya Swala na baada yake, kama walivyosema wanachuoni wengi.

Mwenyezi Mungu alituamuru kuomba dua na akatuahidi kujibu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni.} [Ghafir: 60].

Miongoni mwa Sunna zinazotakiwa kuzifanya wakati wa kuomba dua ni kunyanyua mikono, na kupangusa uso kwa mikono baada ya dua katika Swala na baada yake. Wanachuoni Wa Fiqhi waliafikiana hivyo kama vile Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, Imamu Shafi, Imamu Ahmad Ibn Hanbal. 

Kwani Mtume (S.A.W) amesema: “Mkimuommba Mwenyezi Mungu basi  Muombeni dua kwa viganja vyenu tu, na, mkimaliza kuomba dua panguseni nyuso zenu navyo.” Imepokelewa kutoka kwa Al-Hakim.

Share this:

Related Fatwas