Kutanguliza akili zaidi ya Nukuu.
Question
Je watu wa Al-Ashaaira hutanguliza zaidi mitazamo ya akili kuliko nukuu au wanachukuwa kwenye Qur`ani na Sunna?
Answer
Kauli hii moja kwa moja ni uzushi unaofanywa na maadui wa dhehebu la Al-Ashaaira ili kuchafua sura zao na madhehebu yao, ukweli ni kuwa Ashaaira hutumia akili katika kufahamu nukuu au Andiko, wao hutumia akili na Andiko kwa pamoja, kwa sababu baadhi ya Maandiko hudhaniwa si yenye dalili ya moja kwa moja, hivyo Maandiko haya yanayodhaniwa huyarejesha kwenye uelewa wa kiakili, na kuziacha kwa Mwenyezi Mungu maana zenye shaka, wakati mwingine hufuata mfumo wa maelezo hivyo hutoa ufafanuzi kwa mujibu wa utashi wa lugha na kufahamika maana ya Andiko na muundo wake, ukweli ni kuwa wao katika hilo wametoa huduma kubwa kwenye Uislamu bila ya huduma hizo basi Maandiko yangechukuliwa kwa maana za uwazi wake na kudhani mwenye kudhani kujengewa shaka Mwenyezi Mungu na kudhaniwa kuwa na mwili sawa na sifa za viumbe, kama vile Aya zinazozungumzia mkono mguu na Aya za dalili za hukumu, kama kauli yake Mola Mtukufu:
{Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona} As-Shuura: 11.
Wakazichukuwa Aya ambazo huzaniwa kufananishwa Mwenyezi Mungu na viumbe vyake na kauli yake Mola Mtukufu iliyothibiti hukumu na dalili, hapa ni kufanyia kazi akili katika kufahamu Andiko na kufahamu maana zake kwa sura ambayo inakubaliana katika akili na nafasi ya Muumba.