Kuondoka fidia ya Funga
Question
Wakati gani inaondoka fidia ya funga kwa mgonjwa
Answer
Pindi Muislamu akiwa mkubwa kiumri kwa kiasi ambacho anashindwa kufunga, au anapata tabu sana au madhara, na ameshauriwa na daktari kutofunga kwa sababu ya maradhi ya muda mrefu, na akawa masikini, kwa namna anashindwa kutoa fidia, basi fidia inaondoka kwake Wala halazimishwi kuitoa, kwa sababu fidia inapasa kwa mwenye uwezo mwenye nafasi.