Kuota Katikati ya Funga
Question
Assalaamu Alaiykum .. Ningependa kujua, je, Funga inaharibika kwa mtu kupatwa na janaba akiwa amelala bila ya kukusudia, na hii kwa ndoto inayomjia mwanadamu au vitu vingine vibaya vinavyosababishwa na Shetani.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hapana ndugu muulizaji … kuota katika ya funga hakuharibu funga, mwanadamu anachotakiwa akiamka aoge ili apate kuswali, na hata kama atachelewa kuoga mpaka Magharibi, basi funga yake ni sahihi pia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
