Kusoma surat Al-Akahf Siku ya ijumaa
Question
Je, kusoma surat Al-Akahf Siku ya ijumaa ni suna?
Answer
Kusoma Surat Al-Kahf wakati wowote katika Siku ya ijumaa na usiku wake ni Suna, na inafaa kusoma kwa sauti au kisirisiri.
Sura hii Ina umahususi Siku ya ijumaa, Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. inasema: " Mwenye kusoma surat Al-Akahf Siku ya ijumaa Mwenyezi Mungu atamuangazia nuru chini ya miguu yake mpaka mbinguni itayotoa mwanga Siku ya Kiyama, na atamsamehe madhambi yaliyo kati ya ijumaa mbili" Hadithi hii imepokelewa na Albayhaqy.