Kuapa kuoa katika uchumba
Question
Nimemchumbia binti na shughuli ya uchumba ilihudhuriwa na ndugu wa pande mbili, kisha nikasafiri kwa sababu ninaishi katika mji mwingine. Na tumepanga tarehe ya ndoa mwezi wa tano, na inshaa Allah nitahamia kuishi huko moja kwa moja, na sisi wawili tumeapa kwamba tutaoana na sote tunajua, NK … lakini msichana amebadili msimamo wake ghafla akidai kuwa hana uhakika, hataki matatizo, hataki kuolewa bado. Nimejaribu kumkinaisha hasa kwa sababu sisi tumeapa kwa Mwenyezi Mungu, akaachana na msimamo wake kwa mwezi mmoja, kisha akajaribu tena kuvunja uchumba, na tumeachana kwa njia ya simu, amesema kuwa yeye ameghairi kiapo chake, na tangu kipindi hicho nimekuwa siwezi kuwasiliana naye yeye wala baba yaje. Mama anataka nikachukue zawadi zangu ambazo nilimpa, lakini mimi ninaamini kuwa hilo si katika adabu. Swali: je, niendelee kujaribu kumnasihi na kung’ang’ania kuwa nae au la? Na je, niombe kurudishiwa zawadi zangu? Na je, watu kama hawa wanahesabiwa kuwa ni Wanafiki? Na je, wanatoka katika Uislamu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ndugu yangu.. Uchumba ni ahadi tu ya ndoa, na Mtume S.A.W. anaeleza kwamba Muislamu akitaka kufanya kitu, kisha akakiona kingine bora kuliko kile, basi kunajuzu kwake, kuvunja kiapo chake na kufanya kinyume na kile alichoapa, na kwa hilo, chukulia jambo hilo ni la kawaida na muombe Mwenyezi Mungu hali zenu azifanye nzuri, ima kwa kuwa Pamoja au akuruzuku aliye bora kuliko yeye, na amruzuku yeye bora kuliko wewe, na wala usilifanye jambo kuwa zito, na usimtuhumu mtu unafiki, wala usimkufurishe mtu yeyote katika Waislamu kwa kuwa tu hakutekeleza matakwa yako, lakini juwa kwamba kheri ipo katika kile alichokuchagulia Mwenyezi Mungu, na jua kwamba mapenzi ya kweli ni mtu kutamani kheri kwa anaempenda au aliekuwa anampenda, awe yupo nae au yupo na mwingine, na chukulia jambo hilo ni dogo sana, kwa sababu hujui kheri ipo wapi, na huenda ukaendelea kumfuatilia kumbe jambo halina kheri kwako. Na kuhusu zawadi, ukizitaka hiyo ni haki yako, na ukuiziacha basi hiyo ni kutokana na tabia zako nzuri, na zitamuachia kumbukumbu nzuri.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
