Zawadi za Uchumba
Question
Ni ipi hukumu ya zawadi za uchumba ambazo mchumba wa kiume humpa mchumba wake kipindi cha uchumba?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uchumba, kukubaliwa mahari na zawadi za uchumba ni katika vitangulizi vya ndoa, na ni katika aina za ahadi muda wa kuwa ndoa haijafungwa kwa nguzo zake na sharti zake za kisharia, na kumekuwa na desturi kwa watu kutanguliza uchumba kabla ya kufunga ndoa ili kuandaa mazingira mazuri kati ya familia mbili. Pande moja ikivunja nia yake na ndoa ikawa haikufungwa, basi kisharia mahari inakuwa katika dhima ya mume kwa kufunga ndoa, ikiwa ndoa haikufungwa basi aliyechumbiwa hana haki ya mahari, na mchumba atarudishiwa mahari yake, ama zawadi ya uchumba alizompa mchumba wake, imekuwa ni desturi kuwa hiyo ni sehemu ya mahari; kwa sababu watu wanakubaliana kuoana, na hili linazitoa katika kuwa zawadi na zinakuwa mahari, na desturi imekuwa ikizingatiwa katika sharia ya Kiislamu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili}[Al-Aaraf, 199]. Na imekuja katika athari kutoka Ibnou Masoud Allah amuwie radhi: “Wanachokiona Waislamu ni kizuri basi hicho kwa Mwenyezi Mungu ni kizuri, na wanachokiona kibaya basi kwa Mwenyezi Mungu nacho kibaya”, imetolewa na Ahmad na Al Tayaalisy katika musnad zao, zawadi ya uchumba ni katika mahari, na mchumba ulievunjika uchumba wake, hastahiki mahari kwa sababu si mke, mwanamke anastahiki nusu ya mahari baada ya ndoa, na akishaingiliwa anastahiki mahari yote.
Kutokana na hilo, zawadi ya uchumba inayotolewa na mchumba inakuwa ni ya mchumba akikataa mmoja wao au wote wawili kuoana, na alieyechumbiwa hastahiki kitu chochote, na hilo haliathiri kuwa kuvunja uchumba kuwa kunatoka kwa mwanamke au mwanamume.
Ama zawadi nyingine za kawaida, hizi zinachukua hukumu ya kitu kinachotolewa bure katika fiqhi ya madhehebu ya Hanafi.
yanayofanyiwa kazi hapa Misri; kwa mujibu wa sheria namba 1 ya mwaka 2000 A.D. isemayo: “Na kitu kilichotolewa bure kisharia kinajuzu kutaka kurudishiwa kikiwa kama kilivyo na sifa zake”, hivyo basi, kunajuzu hapa kwa mchumba kuomba arejeshewe zawadi zake za uchumba ambazo matumizi yake hayaishi (Kama pete, heleni na bangili), na ni wajibu kwa aliyechumbiwa kurudisha vitu hivyo.
Ama ikiwa zawadi zinazokwisha matumizi yake (kama vyakula, vinywaji, mavazi) basi havitorudishwa, iwe vitu vyenyewe au tahamani yake; kwa sababu kumalizika ni kuzuizi katika vizuizi vya kurudisha kitu kilichotolewa bure kisharia.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
