Kuweka fedha benki
Question
Ipi hukumu ya kuweka fedha benki?
Answer
Kuweka fedha benki na kuchukua faida zake ni jambo linalofaa Kisharia hakuna dhambi kwenye hilo na wala si katika riba kabisa, bali ni katika makubaliano ambayo yanakubaliana na makusudio halali ya miamala katika Fiqhi ya Kiislamu na kusisitiza uhitaji wa watu kwenye hilo na kusimama kwenye masilahi yao, faida ambazo hutolewa na benki kwa mteja ni ibara ya matokeo ya uwekezaji wa benki fedha za wateja walizoziweka na kuendelezwa, hivyo faida hizi si haramu kwa sababu si katika faida za madeni wala manufaa yanayotokana na makubaliano ya fedha za kujitolea, bali ni ibara ya faida inayotokana na makubaliano ya kufikiwa masilahi ya pande zake.