Kuacha kufanya aqika
Question
Ni ipi hukumu ya kuacha aqika kwa anayeweza kuitekeleza
Answer
Kuacha kufanya Aqika kwa mwenye uwezo ni kukosa thawabu kubwa; Aqika ni Sunna yenye kuhimizwa, na Mtume S.A.W. na ameihimiza sana, na hakuna ubaya kuchinja mnyama mmoja kwa mtoto wa kiume kama ilivyo katika kauli ya Jamhuri ya wanazuoni; katika hili itakuwa sawa kwa mtoto wa kike na wakiume. Akika ameifanya Mtume S.A.W. kwa dalili ya Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibnu Abbas Allah R.A. yeye na baba yake, kuwa Mtume S.A.W. alimchimjia Hassan na Hussein kondoo mmoja mmoja" Hadithi hii imepokelewa na Abou Dawoud. Akimchinjia Mtoto wa kiume wanyama wawili na mtoto wa kike mnyama mmoja inakuwa Bora zaidi.