Kufichua Data ya Wengine

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufichua Data ya Wengine

Question

Ni ipi hukumu ya kufichua data za wengine binafsi kwenye mitandao ya kijamii?

Answer

Hairuhusiwi kufichua data na siri za wengine ambazo hawapendi wengine wazipate; iwe kwenye mitandao ya kijamii, tovuti za kielektroniki au vinginevyo; kwa sababu faragha ya binadamu haijuzu kwa yeyote kuivunja; na matini za kisheria zimetaja kwamba mikusanyiko ya watu ni amana ambayo haifai kufichua kile kilichomo humo ikiwa inajulikana kuwa hilo ni kitu ambacho wamiliki wake hawapendi kufichuliwa; kwa hivyo, kwa yule anayepeleleza faragha hawezi kufichua mpaka ruhusa impewe. Kufichua siri za watu kwa kuonyesha data zao ambazo hawapendi yeyote kuziona ni kitu kinachomletea madhara na hasara, na kudhuru watu ni jambo la kulaaniwa katika dini na inakatazwa na kuonywa kutoka hapo; Mwenyezi Mungu amesema: {Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.} [Al-Ahzab:58].

Share this:

Related Fatwas