Hukumu ya kiokota kinachokutwa na m...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kiokota kinachokutwa na mtumishi wa hoteli

Question

Ni nini hukumu ya kiokota kinachokutwa na mtumishi wa hoteli?

Answer

Inajulikana kisharia kuwa kuhifadhi mali na kutoipoteza au kuiharibu ni lengo mojawapo ya malengo makuu ya sharia ya kiislamu, lakini inawezekana kuwa mmoja amepoteza mali yake na kukutwa na mwingine, hili linajulikna kwa jina la "kiokota" (Luqata), kwa mujibu wa sharia ya kiislamu mali iliyopotea na kutokuwa kwa  mmiliki wake hubaki katika milki yake na huwa ni haki yake yeye, na kwamba linaloruhusiwa ni kuokotwa tu yaani: kuchukua mali ile iliyopotea; kwa lengo la kumtafuta mmiliki wake na kuifikisha kwake, namna za kuifikisha mali inayookotwa kwa mmilika wake ziko nyingi kulingana na mifumo ya kijamii na inayojulikana katika jamii, katika zama hizi za kisasa mali inayookotwa hufikishwa kwa kituo cha polisi ikishindwa kumtambua mmiliki wake, katika suala hili mtumishi wa hoteli anayeokota vitu ndani ya vyumba vya hoteli anapaswa  kuvikabidhi kwa uongozi wa hoteli sawa sawa vitu alivyoviokota ni ghali au la, nayo idara ya hoteli ina haki ya kuchukua hatua na taratibu zinazofaa kwa kuirudisha mali hiyo kwa mmiliki wake.

Share this:

Related Fatwas