Matumizi ya nywele za wanyama katika utengenezaji
Question
Nini hukumu ya kutumia brashi iliyotengenezwa kwa nywele za wanyama?
Answer
Inaruhusiwa kutumia nywele za asili zilizochukuliwa kutoka kwa mnyama. Vile vile hukumu kuhusu sufi zao na manyoya yao na nywele zao, ikiwa ni pamoja na aina zote za matumizi na kuchukua zana mbalimbali kutoka kwao. Na hayo ni kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amekujaalieni majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama nyumba mnazo ziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao na manyoya yao na nywele zao mnafanya matandiko na mapambo ya kutumia kwa muda} [An-Nahl: 80]
Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.