Msimamo wa makundi ya kigaidi kutok...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msimamo wa makundi ya kigaidi kutokana na dhana ya Jihadi

Question

Kwa kiasi gani makundi ya kigaidi yamechafua dhana ya Jihadi katika Uislamu?

Answer

Kwa hakika, makundi ya kigaidi yalitumia dhana ya Jihadi katika Uislamu kimakosa hadi kuchafua dhana yenyewe; ambapo waliibana dhana ya Jihadi kutoka maana pana ya kufanya juhudi za kupambana na matamanio na matakwa ya nafsi kwa ajili ya kuomba radhi za Mwenyezi Mungu wakaitumia kwa maana inayofungamana na vurugu na kufanya jinai za kuua, kuharibu nafsi na mali za wasio na hatia wakiwa Waislamu au wasio waislamu, ni kweli kuwa sheria imekusanya kuwa miongoni mwa maana za Jihadi ni kupigana mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, nawakazanie} [At-Tahrim: 9], lakini Jihadi kwa maana hiyo hairuhusiwi isipokuwa kwa masharti maalumu ambayo ni mengi, na Jihadi kwa maana hii huruhusiwa kimsingi kwa lengo la kujibu uadui na kuwazuia madhalimu wasipite mipaka ya amani na uadilifu, Mwenyezi Mungu Amesema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui} [Al-Baqarah: 190], ikumbukwa kuwa endapo madhara na uadui yanaweza kuzuiwa bila ya mapigano basi Jihadi kwa maana ya mapigano haina sababu kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na wakielekea amani nawe pia elekea} [Al-Anfaal: 61], kwa hiyo, Jihadi kwa maana yake pana huwa wajibu ya waislamu wote wanawajibika kwa makalifisho ya kisheria, kwa sababu hii imeitwa katika Sheria ya kiislamu Jihadi ya juu.

Share this:

Related Fatwas