Visingizio vya makundi ya kigaidi v...

Egypt's Dar Al-Ifta

Visingizio vya makundi ya kigaidi vya kutoa hukumu ya ukafiri.

Question

Ni vipi visingizio vya kutoa hukumu ya ukafiri kwa maoni ya makundi ya kigaidi?

Answer

Kwa kweli makundi ya kigaidi walisawazisha mambo yanayodhaniwa yasiyo na makubaliano na mambo yakinifu yasiyo na shaka, wakazingatia maoni ya viongozi na wafuasi wao misingi ya kuwahukumu watu, wakakataa madhehebu ya kifiqhi na kuwatuhumu watu kwa ufuska wakidai kuwa wanafanya maovu, jambo lililowaongoza kuwakufurisha watu kwa mambo kidhana na tafsiri potofu zinazotegemea ujinga wao na uhaba wa elimu wao, hivyo utawaona wanawahukumu watu kwa ukafiri kwa kuwa wanamwombea Mwenyezi Mungu kwa  baraka za Mtume (S.A.W.) japokuwa jambo hilo limekuja katika Sunna za Mtume, ambapo Mtume alisema akimwelimisha mmoja wa masahaba wake aliyekuja akilalamika upofo: "Akamjia Mtume akasema: ewe Mtume niombee Mwenyezi Mungu Aniponesha, akasema Mtume: ukitaka nitakuombea, na ungesubiri ni bora zaidi kwako, akasema mtu: niombee tu, akamwambia atie udhuu na kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika ninakuomba kwa baraka ya Mtume wako Mohammed Mtume wa rehma, ninakuoomba kwa kutaka shهfaa yake, basi Mola wangu ukubali" (Imesimuliwa na Al-Tirmidhiy) akasema kuwa ni Hadithi hasan sahihi, je, inawezekana kuwa Mtume kuwaelimisha umma wake jambo ambalo halijuzu kisaria au linapoteza imani?!

Share this:

Related Fatwas