Uchi wa baba Pamoja na watoto wake
Question
Ni ipi hukumu ya baba kukaa uchi kabisa mbele ya watoto wake wadogo, na anaweza kufanya hivyo akiwa na umri gani ikiwa inajuzu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu amesema: {Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Swala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Swala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima} [Annur: 58]
Mwanachuoni Ibn Ashur - Mwenyezi Mungu amrehemu - anasema katika tafsiri yake "Al-Tahrir wa Al-Tanwir": "Hizi zilikuwa nyakati ambazo watu wa nyumba walikuwa wakivua nguo zao (maana yake walikuwa wakipunguza baadhi ya nguo), kwa hivyo ilikuwa ni aibu kwa watoto wao kuona sehemu zao za siri, kwa sababu utazamaji huo utawekwa kwenye nafsi ya mtoto, kwani hakuwa na kawaida ya kuziona sehemu hizi za siri, kwa sababu watoto wanapaswa kulelewa juu ya kustiri sehemu zao za siri, mpaka iwe tabia yao ya asili wanapokuwa wakubwa.”
Hii ndiyo adabu kwa watoto: kuwazuia wasione sehemu za siri hadi watakapozoea kustiri wanapokuwa wakubwa.
Mwanachuoni Abu Bakr Al-Jassas amesema katika “Ahkam Al-Quran”: “Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuamrisha mtoto ambaye amezijua sehemu za siri za wanawake kuomba ruhusa mara tatu, akasema: {Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu}. Alimaanisha yule anayejua hilo na kuona sehemu za siri za wanawake, na yule ambaye hakuamrishwa kuomba ruhusa ni mdogo kuliko hivyo.
Hakuna ubaya wa kutojificha mbele ya mtoto ambaye bado hajafikia umri wa utambuzi. Ibn Qudamah Al-Hanbali amesema katika kitabu cha Al-Mughni: “Ama mtoto, maadamu ni mtoto mdogo ambaye bado hajafikia umri wa utambuzi, si lazima kuficha uchi mbele yake kwa namna yoyote ile”.
Sheikh Zakariya Al-Ansari amesema katika kitabu cha “Sharh Al-Bahjah: “Mbele ya mtoto asiyeweza kusimulia anachokiona, inajuzu kufunua sehemu za siri”.
Kwa hivyo, inajuzu kufichua sehemu za siri mbele ya watoto wasioweza kusimulia wanayoyaona. Haijuzu kuacha kuficha uchi mbele ya watoto wenye uwezo wa kueleza wanachokiona. Inajulikana kwamba uangalifu wa watoto kwa mambo haya hutofautiana kulingana na mahali, wakati, mazingira, na watu. Kukataza na kuruhusiwa havifungamani na umri maalumu, bali kwa uwezo wao wa kuelewa, kuelezea, na kuzingatia sehemu hizi za siri. Inapaswa kusisitizwa kwamba kwa kufafanua, kufunua sehemu za siri ni haramu kwa kauli moja. Na kabla ya umri wa utambuzi, inafaa zaidi na yenye murua na inamfaa zaidi kujiepusha na kufichua uchi pasipo na haja, hasa ikiwa uelewaji wao unaanza kusitawi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
