Hatari ya kuuondoa mtaala wa Al-Azh...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hatari ya kuuondoa mtaala wa Al-Azhar katika maisha ya Waislamu na athari zake

Question

Kuna hatari gani ya kuuondoa kwa mtaala wa Al-Azhar katika maisha ya Waislamu na athari zake?

Answer

Hatutii chumvi tunaposema kwamba kuuondoa mtaala wa Al-Azhar katika maisha ya Waislamu ni kifo cha roho ya Uislamu katika nafsi zao, na kuenea kwa machafuko ya kidini. lakini sababu kuu ya kuibuka misimamo mikali na ugaidi ni umbali kutoka kwa mtaala wa Al-Azhar katika kujifunza na kufundisha dini na ulinganiaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hii ni kwa sababu mtaala wa Al-Azhar Al-Sharif ni mtaala wa Ahlul-Sunnah wal-Jama'ah. Kuondoa mtaala huu ni kuondoa kwa mitaala ya Kisunni, na kadiri kasoro inavyotokea katika utekelezaji wa mtaala wa Al-Azhar kwa Waislamu, kuna kasoro katika dini yao, na dosari katika dini ya Muislamu na ndiyo ni kasoro katika ulimwengu wake na Akhera yake, na mtaala wa Al-Azhar au mtaala wa Ahlul-Sunnah unategemea nguzo kuu tatu. Nazo ni, kwa mpangilio: Itikadi ya Ahlul-Sunnah wal-Jama'ah (imani ya Ash'aris, Maturidis, Wanazuoni wa Hanbali), Kushikamana na moja ya madhehebu manne ya kifiqhi yanayofuatiwa, nayo ni (Hanafi, Maliki, Shafii, Hanbali), na kufuata usufi kama ni njia ya kujielimisha na kufika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa mujibu wa haya wanazuoni watangulizi na waliokuja baadaye tangu zama zilizopita mpaka wakati wetu huu, na sifa njema ni za Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Share this:

Related Fatwas