Tofauti kati ya mapenzi wanayodai w...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti kati ya mapenzi wanayodai wenye itikadi kali na mapenzi ya Waislamu kwa Mtume S.A.W.

Question

Ni ipi Tofauti kati ya mapenzi wanayodai wenye itikadi kali na mapenzi ya Waislamu kwa Mtume S.A.W. 

Answer

Mapenzi ni utashi pamoja na nafsi kukubali na kumili katika inachokiamini, na dalili ya mapenzi ya kweli ni kumtii unayempenda na hakuna vingine, na katika hilo kuna msemo wa baadhi ya washairi:

Unamuasi Mola hali yakuwa unadhihirisha mapenzi yake*

Naapa hili ni jambo baya sana katika kipimo cha mapenzi

Lau mapenzi yako yangekuwa ya kweli ungemtii*

Kwa hakika mpenzi ni mtiifu kwa ampendae.

Na mapenzi ya Waislamu kwa Mtume S.A.W. ni katika mapenzi yao kwa Mwenyezi Mungu, Mtume S.A.W. amesema: “Mpendeni Mwenyezi Mungu kwa neenma zake anazokuneemesheni, na nipendeni mimi kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na wapendeni jamaa zangu kwa mapenzi yangu” [Hadithi hii ameipokea Al-Timidhy] na hakukuwa Kudumu Waislamu katika Sunna za Mtume S.A.W, kuwapenda jamaa za Mtume, kusheherekea Maulid na kufurahi kwa kumsifu, kufanya vikao vya kumswalia Mtume na kutawassul kwa cheo chake kitukufu na  kuwanyenyekea kwao viumbe isipokuwa ni kuakisi kudhihirsha mapenzi haya katika matendo yao, hivyo kuna tofauti kubwa kati ya mapenzi haya na mapenzi ya watu wanaoharamisha kusheherekea Mauli  na kukataza kufanyika vikao vya kumswalia Mtume S.A.W. wala wahawafurahii kusifiwa kwake, na wanasema Kutawassul kwa Mtume ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu! Haya ni mapenzi gani wanayoyadai?!

Share this:

Related Fatwas