Madhara yatokanayo na Khawariji wa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Madhara yatokanayo na Khawariji wa kisasa katika haiba ya umma, maisha ya kijamii na Kidini nchini Misri

Question

Jinsi gani Khawariji wa kisasa wameharibu au wamedhuru haiba ya uma, maisha ya Kijamii na kidini Misri?  

Answer

Minhaji ya Khawariji ya kisasa imekuwa ya kipekee kwa baadhi ya fikra zisizo za kawaida wameawahadaa watu kuwa fikra hizo ni katika dini, miongoni mwao ni migogoro endelevu na serikali na kudai kwamba serikali zote zinazoongoza Ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa ni serikali za kidhalimu kama si za kikafiri, kwamba sharia haitekelezwi katika miji yetu, sambaba na kueneza uzushi na uongo ambao lengo lake ni kuwasha moto wa fitina kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu miongoni mwa raia wa nchi moja, na misingi hii imeakisi matendo ya baadhi wa watu ambao wamesadikisha uongo na uzushi wao, tunakuta baadhi yao wanahalalisha mali ya umma kwa kile walichokiona kuwa ni udhalimu au ukafiri wa serikali, na wala hawarudi kwa Wanazuoni wa taasisi zilizo rasmi, bali wanawadharau na wanachukia ndugu zao katika ubinadamu na utaifa, hawafanyi nao miamala, na mengineyo mengi ambayo yapo mbali na Dini sahihi na pia tabia njema.     

Share this:

Related Fatwas