Juhudi za Ofisi ya Mufti wa Misri k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Juhudi za Ofisi ya Mufti wa Misri katika kupambana na Itikadi kali na Ugaidi

Question

Ni zipi Juhudi za Ofisi ya Mufti wa Misri katika kupambana na Itikadi kali na Ugaidi?

Answer

Ofisi ya Mufti wa Misri ni taasisi kongwe ya kitaifa, inafuata njia ya kielimu ya ukati na kati wa ustahamala unaoelezea uzuri wa Uislamu, na katika nukta hii Ofisi ya Mufti ikatanabahi hatari za fikra za harakati za itikadi kali tangu awali, na ikafanya juhudi ili kupambana na fikra hizo zisizo za kawaida na Fatwa ngeni katika Dini yetu Tukufu. Yakawa malengo makubwa ya (Sekretarieti Kuu ya ofisi na mamlaka za Fatwa Ulimwenguni) Ambyo Ofisi ya Mufti ya Misri ilifanya juhudi kubwa ili kuanzishwa kwake: kupiga vita fikra za wenyeitikadi kali, na kuimarisha Manhaji ya ukati na kati katika Fatwa. Pia Ofisi ya Mufti ya Misri ilianzisha (Mtandao wa kufuatilia Fatwa za Kukufurisha na rai za itikadi kali) miongni mwa kazi za mtandao huo ni: kufuatilia kauli za makundi ya kukufurisha katika mitandao ya kijamii video na machapisho, kutoa msaada kamili kwa taasisi za Fatwa na njia za kupambana na milipuko ya kifkra hizo. Na juhudi za hivi karibuni za Ofisi ya Mufti ya Misri ni kuanzisha (Kituo cha Amani cha tafiti za Itikadi kali),  na kupitia idara na vituo kama hicho na vinginevyo Ofisi ya Mufti ya Misiri inaingiliana na hali ya maisha kwa ngazi zote za kielemu na kifikra ili kutoa kilichobora iwezekanavyo katika upande huu kwa wanadamu wote Ulimwenguni kote.

Share this:

Related Fatwas