Ufinyu wa Uelewa na udhaifu wa maon...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ufinyu wa Uelewa na udhaifu wa maoni Unapelekea itikadi kali na Ugaidi

Question

Jinsi gani Ufinyu wa Uelewa na udhaifu wa maoni unasabaisha itikadi kali na Ugaidi?

Answer

Miongoni mwa sifa za fikra yenye itikadi kali ni ufinyu wa Uelewa, na Maandiko mengi ya kisharia yakitazamwa kwa juu juu basi matokeo ni kwenda kinyume na makusudio ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika Maandiko hayo, mfano wa wazi katika hilo ni maana ya Bidaa kwa watu wenye itikadi kali, kwani kauli ya Mtume S.A.W.: “Na Shari ya mambo ni uzushi wake, na kila Bidaa ni upotevu” [Ameipokea Muslim], wameichukulia kwa kila jambo lililozushwa hakulifanya Mtume S.A.W. basi ni Bidaa na upotevu, wakajibana wao wenyewe na kuwabana watu. Mtume S.A.W. hakukusudia hilo, Masahaba hawakuelewa hivyo, Qur`ani Tukufu ilikusanywa katika msahafu mmoja baada ya kufariki Mtume S.A.W. Omar bin Al-Khattab R.A. aliwakusanya Waislamu nyuma ya Imamu mmoja katika Swala ya Tarawehe, na akasema: “ Bidaa nzuri ni hii”[Al-Muattaa], na Imamu Shafi ambaye  ni miongoni mwa Maimamu wema waliotangulia ameelezea kuigawa Bidaa katika: Nzuri, na mbaya, lakini ubishi wa upofu umewazuia wenye itikadi kali kufuata haki na kuwazibia njia.

Share this:

Related Fatwas