Msimamo wa Uislamu juu ya misimamo ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msimamo wa Uislamu juu ya misimamo mikali na itikadi kali.

Question

Nini msimamo wa Uislamu kuhusu msimamo mkali na itikadi kali?

Answer

Suala la kukabiliana na misimamo mikali ni moja ya masuala muhimu yenye hatari kubwa, kwani hatari yake inatishia usalama na utulivu wa umma katika jamii, na sura zake ni pana na athari zake ni nyingi katika maisha yetu ya kila siku. Misimamo mikali hii ilisababisha kuchochea ghasia hadharani, ambapo vyombo vya habari, sauti na magazeti vilichangia, pamoja na mitaala ya elimu katika baadhi ya nchi, mihadhara na baadhi ya hotuba potovu za kidini zenye msimamo mkali. Madhehebu na sura za kidini zenye msimamo mkali pia zilichangia katika kuchochea misimamo mikali, kwa sababu ya ushawishi wao mashuhuri juu ya maisha na tabia za baadhi ya watu na harakati.

Ni muhimu kusisitiza kuwa misimamo mikali haiwezi kuzuiliwa kwa kundi au eneo fulani pekee. Inabainika kuwa sehemu inayoonekana ya watu wenye msimamo mkali ni wale ambao ni wa makundi ya kigaidi, lakini ukweli ni kwamba misimamo mikali inaenea ndani ya makundi mengi katika jamii ambayo haionekana  kwa uwazi.

Uislamu ulileta upole na kustahamiliana na kutaka kuwepo kwa uwastani katika mambo yote. Uislamu daima umeegemezwa juu ya uvumilivu, kukubali wengine, na kukataa misimamo mikali na itikadi kali. Kwa hiyo, Uislamu ulichukua msimamo wazi, wenye maamuzi dhidi ya misimamo mikali na itikadi kali. umetaka kukataliwa kwake, kujiweka mbali na kupinga.

Share this:

Related Fatwas