Fatwa za watu wa misimamo mikali.

Egypt's Dar Al-Ifta

Fatwa za watu wa misimamo mikali.

Question

Mara nyingi watu wa ukufirishaji hupitisha Fatwa zisizofanyiwa tafiti na si zauadilifu, tafadhali elezea hilo 

Answer

Watu wengi wenye misimamo mikali hutoa Fatwa bila ya kuwa na hata chembe ya sifa ya kazi hiyo, wanafanya hivyo kueneza Fatwa za kiuchochezi na kuziunda tena kwenye ndimi zao, ili waweze kufanya vitendo vya misimamo mikali kwa njia ya kupanua wigo wa haramu, hakuna shaka kuwa hilo linawaingiza katika matatizo mengi, miongoni mwayo:

Msimamo mkali.

Nayo ni sifa maalumu ya mtu wa msimamo mkali, ambapo mtu wa msimamo mkali huimarisha juhudi zake ili kulinda kile anachoshikamana nacho na kuamini katika fikra zake, naye ni mwenye msimamo mkali pia anapoteza ulaini na uwezo wa ushirikiano wa kijamii.

Kuwaangalia wapinzani wao na wakosoaji wao kuwa kwa asili ni watu wabaya.

Wapinzani kwa upende wa watu wa misimamo mikali hawakuwa isipokuwa ni watu waovu hawana maadili, waliokosa usafi wa nafsi na uaminifu, kama vile wanawaona watu wa chuki, wenye mioyo migumu na tabia mbaya, hilo si kwa vile tu hawakubaliani na wao katika kauli zao imani na tabia zao, bali pia ni kwa sababu wanaona mambo kwa njia tofauti na wana umuhimu unaopingana na umuhimu wao.

Mvutano wa hisia kila wakati.

Mtu wa msimamo mkali siku zote yuko katika hali ya hasira, naye hurithi mgongano katika hali yake ya hisia kuongezea kuwa na wasiwasi ambao anaishi nao na kuwa nje ya vipimo vya kijamii na kudharau mfumo misingi mila na desturi zilizopo kwenye jamii.

Share this:

Related Fatwas