Akili za watu wa misimamo mikali.

Egypt's Dar Al-Ifta

Akili za watu wa misimamo mikali.

Question

Zipi sifa kuu zenye kuathiri akili ya mtu wa msimamo mkali?

Answer

Akili ya mtu wa msimamo mkali na misimamo mikali inasifa kadhaa zenye kuathiri maandalizi yake kifikra kitamaduni na katika kuhama kwake katika hatua za misimamo mikali, na sifa hizo kuu:

Ufuasi wa watu wa fikra kali unatangulizwa zaidi ya ufuasi wa fikra yenyewe, ufuasi wa watu wenye kufuata vikundi vya kigaidi hutangulizwa zaidi ya kufata kwao Uislamu, ambapo ufuasi wa vikundi ndio asili, na ufuasi wa Uislamu ni tawi.

Kushikamana na fikra za zamani na kuzitakasa pamoja na kupinga kila kilicho kipya au kupambanua kati ya kosa na baya katika anayobeba.

Mfumo wa kimakabiliano na vikundi vyote pamoja na fikra mbalimbali, ni sawa sawa vikundi hivyo vikiwa vinafuata dini hiyo hiyo au kabila au hapana.

Kuchafua ukweli: Nayo ni sifa inayotoa uwezo wa kupindua maana, na kutanguliza dalili zisizotosheleza au zinazopingana na hali halisi.

Kujifungia kwenye nafsi na kupinga fikra yeyote iliyo kinyume hata kama itakuwa ni sahihi.

Kukosekana fikra ya kukosoa, hilo hapo baadaye huwageuza watu wa hayo makundi ya msimamo mkali na kuwa wachache wenye fikra zilizoganda zisizoboreka, kutokana na hilo huzaliwa utukuzaji wa viongozi wa vikundi.

Kukosekana fikra ya mazungumzo na usamehevu, jambo linaloimarisha fikra za ukufirishaji, na kuasisi hapo baadaye mitazamo ya vitendo vya matumizi ya nguvu.

Share this:

Related Fatwas