Juhudi za serikali ya Misri katika ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Juhudi za serikali ya Misri katika kupambana na ugaidi na itikadi kali.

Question

Nini juhudi za serikali ya Misri katika kupambana na ugaidi na itikadi kali?

Answer

Taifa la Misri linafanya juhudi kubwa zaidi za kupambana na ugaidi na misimamo mikali katika ngazi zote. Katika ngazi ya usalama, vyombo vya usalama vya Misri vinafanya kazi hii kwa ukamilifu zaidi, kwa kufuatilia, kukata njia za kuenea, na kupambana kwaumakini, na ushujaa uliosajiliwa katika historia. Katika ngazi ya kijamii, mamlaka zinazohusika husaidia familia za waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi na kuwasaidia kifedha na kimaadili, na wale wote walioathiriwa na hatua za kukabiliana na ugaidi hufidiwa kwa hasara zao zote. Ama kuhusu kiwango cha kielimu na kifikra, taasisi za kidini - zinazoongozwa na Ofisi ya Fatwa ya Misri - zinafanya jambo hili na kutekeleza wajibu wao kwa dini na nchi. Taasisi hizo zimezindua vituo kadhaa vya uchunguzi na vituo vinavyofanya kazi ya kupambana na maoni na Fatwa za kidini zenye msimamo mkali, kueneza mawazo ya wastani yaliyoelimika, na kuongeza ufahamu miongoni mwa vijana. Kwa kutumia mbinu na njia zote, hasa mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali, misafara na mipango mingi ya kielimu na kiulinganiaji na kufanyika kwa makongamano yanayoshughulikia suala hili.

Share this:

Related Fatwas